September 27, 2019


Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Eliuter Mpepo anayekipiga katika timu ya Buildcon ya Zambia amefunguka kuwa Yanga wanayo nafasi ya kuibuka na ushindi dhidi ya Zesco United ikiwa imefanya maandalizi makubwa kutokana ukubwa wapinzani wao.

Timu hizo zinatarajiwa kucheza mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika, kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Levy Mwanawasa uliopo Ndola, Zambia, baada ya sare ya bao 1-1 ya katika mchezo wa kwanza.

Mpepo amesema kuwa Yanga wanaweza kupata matokeo ya ushindi ikiwa wamejiandaa vizuri kutokana na wapinzani wao kutokuwa na rekodi ya kufungwa kwenye uwanja wao nyumbani.

“Unajua mchezo wa soka upo tofauti na unavyoongelewa kwa sababu ukiangalia Zesco hawajawahi kupoteza mchezo wakiwa kwenye uwanja wa nyumbani, jamaa wanakuwa na wakali sana jambo ambalo Yanga wanapaswa kulielewa.

“Lakini nafahamu ukubwa wa Yanga na kama watakuwa wamejiandaa basi wanaweza kupata matokeo kitu ambacho kinawezekana kwa kuwa soka ni mchezo wa makosa na Yanga hakuna asiyejua kwamba ni wazuri zaidi wanapokuwa ugenini ingawa ina wachezaji wengi ambao bado ni wapya,” alisema Mpepo.

5 COMMENTS:

  1. Hata wafanye nini kipigo kipo pale pale. Wapunguze magoli tu.

    ReplyDelete
  2. Tunangojea visingizio. Hakuna cha meza wala tema .Kufungwa tena sio chini ya goli 2.

    ReplyDelete
  3. eti tuna taka kwenda world cup, wakati hata hatuna na imani na timu zetu.

    ReplyDelete
  4. Msilazimishe uzalendo wakati mnaukataa mara kwa mara.Kufeni na lwenu.Kila moja ashangalie timu yake.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic