VITA ya magolikipa wawili wa KMC ambao wote wanazitumikia timu zao za Taifa leo imemalizika uwanja wa Taifa kwa mmoja kuibuka mbabe baada ya kuipeleka timu yake hatua ya makundi.
Juma Kaseja mlinda mlango wa Tanzania anayekipiga klabu ya KMC na Jonathan Nahimana wa timu ya Taifa ya Burundi ambaye aliingia akichukua nafasi ya Justin Ndikumana dakika ya 119.
Kwenye mchezo wa leo wa kutafuta tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar baada ya Kaseja kuokoa penalti moja na mbili wapigaji wa Burundi kukosa.
Kwa upande wa Tanzania mfunguzi alikuwa ni Erasto Nyoni kisha Himid Mao na msumari wa mwisho ukapachikwa na Gadiel Michael.
Tanzania inasonga mbele kwenye hatua ya makundi Kwa Ushindi wa penalti 3-0 baada ya dakika 120 kukamilika Kwa kufungana bao 1-1.
Ikumbukwe kuwa mchezo wa kwanza uliochezwa nchini Burundi timu zote zilitoshana nguvu Kwa kufungana bao 1-1.







NI UKWELI USIOPINGIKA BILA UNAFK KASEJA NDO "TANZANIA ONE" PEKEE HONGERA TAIFA STARS MUMECHEZA VZUR NA MUMEPAMBANA. HAKIKA TUTAFKA MBALI NA TUNAZD KUWAOMBEA MASHUJAA WETU.
ReplyDeletekacheza vizur kaseja lkn ifike watat tuanze kuwaamini na makipa wengne ili wapate uzoefu kama J.K.J
ReplyDelete