KUELEKEA kwenye
mchezo wa kimataifa wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na Zesco
unaotarajiwa kuchezwa Septemba 14 uwanja wa Taifa, tayari mlinda mlango, Farouk
Shikalo amepata kibali cha kushiriki michuano ya kimataifa.
Shikalo
ambaye amejiunga na Yanga akitokea timu ya Bandari alikosa michezo miwili ya
kimataifa dhidi ya Township Roller na langoni alikaa Metacha Mnata jambo
litakaloongeza ugumu wa namba ndani ya kikosi.
Kaimu Katibu wa Yanga, Dismas Ten amesema kuwa utaratibu wa kukamilisha
kibali kwa Shikalo umefikia hatua nzuri na wana imani ya kumtumia kwenye mchezo
dhidi ya Zesco.
“Kwa sasa
mipango inaendelea vema kuelekea mchezo wetu dhidi ya Zesco na tayari
tumekamilisha hatua zote za kupata kibali rasmi cha kumtumia Shikalo kwani kila
kitu kipo sawa.
“Kinachosubiriwa
kwa sasa ni uthibitisho rasmi kutoka kwa Caf juu ya kumtumia mchezaji wetu
Shikalo kwenye mechi ya marudio huku na wengine tukiendelea kufuatilia taarifa
zao.” amesema Ten.
Wachezaji
wengine ambao vibali vyao vinafuatiliwa na walikosa mchezo dhidi ya Township
Rollers ni pamoja na David Molinga ‘Mwili Jumba’ na Maybin Kalengo.








Hivi ni udhaifu wa kiutendaji ama ni nini? Kwanini inachukua muda mrefu kupata CAF licensing as wachezaji wa Yanga pekee na sio Azam???
ReplyDeleteHizi taarifa kuna muda zinachanganya
ReplyDelete