RODWELL Chinyengetere
mshambuliaji wa FC Platinum aligeuka mwiba mkali kwa wapinzani wake UD do Songo
ambao waliitoa Simba kwenye hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kuwafungashia
vilago kwenye Ligi ya Mabingwa sasa watashiriki kwenye Kombe la Shirikisho
baada ya kutolewa kwa jumla ya mabao 5-1.
UD Songo iliitoa Simba kwa
faida ya bao la ugenini baada ya mchezo wa kwanza kulazimisha sare ugenini na
mchezo wa pili kutoka sare ya kufungana bao 1-1 uwanja wa Taifa.
Mchezo wa kwanza Ud Songo ilikubali kichapo cha bao 1-0, kabla ya juzi kukubali kichapo cha mabao 4-2 Uwanja wa Estadio do Ferroviario na Chinyengetere kuwa shujaa wa mchezo kwa kusepa jumla na mpira wake baada ya kufunga hat trick.
FC Platinum inasonga hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika huku wabaya hao wa Simba, UD do Songo wakitupwa jumla kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho.
0 COMMENTS:
Post a Comment