AZAM FC mabingwa
watetezi wa Kombe la FA, wamekubali yaishe kwenye michuano ya Kimataifa baada
ya kutolewa na Triangel United kwenye Kombe la Shirikisho hatua ya awali.
Azam FC iliyo chini ya
Kocha Mkuu, Ettiene Ndayiragije imefungashiwa virago baada ya kufungwa jumla ya mabao 2-0 na wapinzani wao Triangle United ambao
waliifunga nje ndani.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Maganga amesema kuwa
hesabu zao ilikuwa kupindua meza kibabe wamekwama hivyo wanarejea kujipanga kwa
ajili ya wakati mwingine.
“Tulipambana kwa ajili
ya kutafuta matokeo na mipango yetu ilikuwa ni kupindua meza bahati haikuwa
yetu kwa sasa tunarejea Bongo kuendelea kujipanga kwa ajili ya michezo ya Ligi
Kuu Bara,” amesema Maganga.
Hiyo kupinduwa meza kibabe ndiyo iliyowadhuru watani
ReplyDelete