September 28, 2019



KIUNGO wa kimataifa wa Zesco United ya Zambia, Anthony Akumu raia wa Kenya amefichua kuwa wamejipanga vizuri kuisambaratisha safu ya kiungo ya Yanga inayoongozwa na Papy Tshishimbi na Abdulaziz  Makame kwa kuwa ndiyo walikuwa kikwazo kwao.

Akumu ametoa kauli wakiwa kwenye maandalizi yamwisho ya mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika  dhidi ya Yanga utakaopigwa leo nchini Zambia baada ya kutoka sare ya 1-1 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar.

 Akumu amesema tayari wameshaanza wamejipanga vizuri kuhakikisha wanapata matokeo ya ushindi katika mchezo wa marudiano kwa kuwa wameshatambua udhaifu wa wapinzani wao.

“Tunaendelea  na maandalizi tunatambua kwamba wapinzani wetu Yanga walitubana zaidi kwenye eneo la kati hivyo tunajipanga kufanya vema.

 "Unajua katika kipindi cha kwanza  wao walichofanya kwa eneo la kati ni kumtumia yule mwenyewe namba 21 (Makame) ambaye alikuwa akitokea pembeni kuja kati kuvuruga na hata yule nahodha wao (Tshishimbi) maana muda mwingi walifanya kati kuwe kugumu lakini naamini kwa maandalizi yetu ni lazima tushinde,” amesema Akumu.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic