CAF YAWATENGENEZA YONDANI, LAMINE YANGA
Wakisubiria droo ya Kombe la Shirikisho Afrika kesho Jumatano, Kocha Msaidizi wa Yanga, Mzambia Noel Mwandila ameahidi kuisuka upya safu mpya ya ulinzi ya Yanga inayoongozwa na Mghana, Lamine Moro na Kelvin Yondani.
Hiyo, ni baada ya timu hiyo kupata matokeo ya sare ya mabao 3-3 walipocheza mchezo wa pili wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Polisi Tanzania kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam wiki iliyopita.
Huo ni mchezo wa pili Yanga kuruhusu mabao, mwingine wa kwanza walifungwa bao 1-0 na Ruvu Shooting kwenye uwanja huo.
Mwandila alisema safu hiyo ya ulinzi imefanya makosa kwenye michezo miwili, hivyo inahitajika kuboreshwa kabla ya kwenda hatua ya mtoano ya shirikisho.
Mwandila alisema ana matarajio makubwa kuwa safu hiyo ya ulinzi itaimarika.
“Safu yetu ya ulinzi haikucheza vizuri katika michezo miwili ya ligi ambayo tumeicheza baada ya kuruhusu mabao manne kwenye michezo miwili ya ligi.
“Mfano kwenye mchezo wetu wa ligi tulipocheza na Polisi Tanzania kipindi cha kwanza tukiwa tunaongoza timu haikucheza vizuri kabla ya kusawazisha na baadaye wakatuongeza mabao mengine mawili na kusawazisha.
“Hivyo, basi tumepanga kuendelea kuisuka upya safu ya ulinzi ili icheze vizuri kwa kuelewana tukielekea kwenye Kombe la Shirikisho,” alisema Mwandila.
0 COMMENTS:
Post a Comment