October 28, 2019


Baada ya kichapo cha jana dhidi ya Pyramids FC katika mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika, Yanga imejiwekea wakati mgumu wa kutwaa milioni 30 za kampuni ya GSM ambao ndiyo wadhamini wao.

Yanga imejiwekea wakati mgumu kufuatia kupoteza mechi ya kwanza hapa nyumbani baada ya kufungwa mabao 2-1.

Kupoteza kwa Yanga kunaleta ugumu wa kujinyakulia fedha hizo katika mechi ya marudiano ambayo itafanyika Misri.

Njia pekee ya Yanga kuzibeba milioni hizo ni kupindua matokeo ugenini hali ambayo kiuhalisia inaonesha itakuwa ngumu kutokana na timu za kiarabu zikiwa kwao inakuwa ngumu kuzifunga.

baada ya mechi hiyo, Yanga sasa itakuwa inajiandaa na mechi za ligi pamoja na Ligi Kuu Bara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic