IBRAHIM
Ajibu, Kiungo mshambuliaji wa Simba ambaye amejiunga msimu huu kwa kandarasi ya
miaka miwili akitokea Yanga ametumia dakika 139 kujibu maswali ya mashabiki
juu ya uwezo wake alionao.
Msimu
uliopita akiwa ndani ya Yanga, Ajibu alikuwa ni kinara wa kutoa pasi za mwisho
ambapo alitoa 17 na alianza kwa kutoa asisti tatu na kufunga bao baada ya dakika 90 kwenye mchezo dhidi ya
Stand United na Yanga ilishinda mabao 4-3 uwanja wa Taifa jambo lililoacha
maswali kwa mashabiki kama nyota huyo ataweza kuonyesha makeke ndani ya Simba.
Tayari
ameshaanza kuonyesha makeke yake ambapo kwenye jumla ya michezo mitatu ambayo
amecheza ameweza kutumikia timu yake ndani ya dakika 162 na asisti yake ya
kwanza ameitoa dakika ya 55 kwenye mchezo dhidi ya Biashara United
lililopachikwa na Miraj Athuman.
Hivyo maswali
ambayo walikuwa wanajiuliza mashabiki tayari ameanza kuyajibu akiwa ndani ya
Simba, kwani kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania aliocheza kwa dakika 13, Kagera Sugar dakika 71 hakuweza kujibu ila
moto aliuwasha alipopewa dakika 77 alipocheza na Biashara United na Simba
iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.
0 COMMENTS:
Post a Comment