October 9, 2019


Beki wa klabu ya Simba, Kennedy Wilson ameibuka na kusema changamoto kubwa anayokutana nayo ndani ya kikosi cha timu hiyo ni mawasiliano baina yake na Wabrazil Tairone Santos da Silva pamoja na Wilker da Silva.

Beki huyo aliyesajiliwa kutoka Singida United, ameeleza imekuwa shida kuelewana na wachezaji hao wakiwa nje ya uwanja kwani hawajui lugha ya Kiswahili wala Kiingereza.

Kennedy amefunguka kuwa kutojua kwao lugha hizo mbili na yeye kutokifahamu Kibrazil inakuwa ni ngumu kwake kukaa kisha kupiga nao stori za hapa na pale sababu hawawezi kuelewana.

Mbali na kutoelewana wakiwa nje ya uwanja, Wilson ameeleza pindi wanapokuwa ndani ya uwanja wanaelewana vizuri sababu lugha ya mpira inaeleweka.

"Changamoto kubwa imekuwa ni kuelewana na Tairone pamoja na Santos sababu hawajui Kiswahili wala Kiingereza.

"Inakuwa ngumu kukaa pamoja halafu tupige stori tunapokuwa nje ya uwanja sababu mimi pia sijui Kibrazil, mbali na hapo tukiwa uwanjani tunaelewana vizuri sababu lugha ya mpira inaeleweka.

"Fraga yeye anaelewa Kiingereza hivyo inakuwa rahisi kwangu kuzungumza naye."

Tangu atue Simba akitokea Singida United, Wilson amecheza mechi moja pekee ya Ligi Kuu ambayo ilikuwa dhidi ya Biashara United waliyoshinda mabao 2-0 huko Musoma, Mara.

2 COMMENTS:

  1. Nadhani maeleweano ya mpira ni mpira.Yaani beki mwenye kujua na kujiamini na kazi yake sizani kama lugha ni kikwazo cha kumzuia kuonesha uwezo wake. Alikuja chama na ugeni wake lakini akatoboa.Kama vile haitoshi kaja msudani Ashraf kuingia tu uwanjani watu wamepagawa. Vijana wetu wanatakiwa kuondosha uoga na kujifunza kwa haraka. Kwanini aliletwa kahata simba? Sababu akina Ndemla wanasubiri labda mpaka wawe wazee ndio waje kuamka. Kwani simba au kocha wao wanahamu sana hivi sasa kutafuta fowadi nyengine hasa ya kigeni? Jibu hapana .Sababu? Miraji Athumani anafanya kazi inayostahiki kufanywa pale mbele. Kwani Simba ilihangaika kutafuta kipa wa kigeni? Jibu hapana. Sababu? Manula anafanya kazi inayostahiki kufanywa pale golini.Na yeye Kenedi bado hajatosha au hajajitambua lakini ikitokezea siku akiidhibiti vilivyo nafasi yake ya beki wa kati pale simba basi sio yeye tena atakaehangaika kujifunza lugha ya mchezaji mwenzake wa kigeni bali wageni watalazimika kujifunza kutoka kwake. Ni ujumbe mfupi kwa Kennedy na wale wote wachezaji wazawa. Kwani ulishawahi kumsikia Kevin Yondani akilia na ugumu wa lugha?

    ReplyDelete
  2. Irudie mada juu uisome tena, mwandishi kasema nje ya uwanja na sio ndani ya uwanja. Kuna maisha wanaishi wachezaji nje ya uwanja ya kawaida kama unavyoishi ww na jirani zako. So lugha ni barrier kwao kuweza kuzungumza kama unavyozungumza ww na rafiki zako. Ulichokiongea ni kweli but kwa mtazamo wangu umeenda tofauti na alichokisema Kennedy

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic