October 28, 2019


ETIENNE Ndayiragije, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa amesema kuwa kikubwa anachokiomba kwa sasa ni ushirikiano ili kufikia malengo makubwa.
Ndayiragije amepewa kandarasi ya mwaka mmoja kuiongoza timu ya Stars baada ya kutimiza mashari aliyopewa wakati akikaimu nafasi hiyo kwa kuipeleka timu hatua ya makundi ya Kombe la Dunia pamoja na kufuzu michuano ya Chan itakayofanyika 2020 nchini Cameroon.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ndayiragije alisema kuwa kikubwa kinachohitajika kwa sasa ni kuendeleza ushirikiano ambao ulikuwepo tangu awali wakati akiinoa timu ya Taifa.
“Kila majukumu yana ugumu wake na muhimu katika kukamilisha mipango ni ushirikiano ili kufikia malengo ambayo tumejiwekea kwani kufikia mafanikio sio jambo la mara moja.
“Kuna mengi makubwa tunafikiria kuyafanya ila haitawekeana kama hakutakuwa na ushirikiano nina amini kila kitu kitakuwa sawa kwani kuna vipaji vingi nimeviona,” alisema Ndayiragije.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic