October 6, 2019






NANI wa kulaumiwa baada ya timu zetu nne kutofanya vizuri kwenye michuano ya klabu barani Afrika msimu huu?
Swali lingine, tumejifunza nini kwa hilo lililotokea kwa timu zetu kutofanya vizuri?

Hayo ni maswali mawili magumu na mepesi kuyajibu ila sina hakika kama wajibu wako tayari kuyajibu au kutoa majibu sahihi.

Waswahili wanasema kwenye miti hakuna wajenzi ndio kama ilivyotokea kwa klabu zetu pamoja na kupewa bonasi hiyo ya timu nne, lakini wapi tumeshindwa kuitumia.

Wenzetu wanazitamani sana hizo nafasi nne, lakini sisi tumezipata na tumeishia kuzichezea tu.

Pamoja na kutolewa mapema, timu zetu zote nne hazikuwa kwenye kiwango bora cha kujivunia eti zinaweza kuleta kitu kutoka kwenye michuano ya klabu za Afrika.

Hapo juu nimesema tumejifunza nini baada ya timu zetu kutolewa mapema, kiukweli sina hakika kama kuna watu wamejifunza.

Mara nyingi tumekuwa tukijitetea kwa kusema eti tunajifunza au tunajenga timu, yaani hizo kauli sitaki hata kuzisikia.

Sitaki kuzisikia, unajua kwa sababu gani? Kwa sababu sio kweli kama tunajifunza au tunajenga timu, bali ni longolongo tu hatuna mpya.

Msimu uliopita nilimuambia rafiki yangu mmoja unajua kuna timu kutinga hatua ya makundi ni jambo la kawaida kutokana na mfumo wao waliojijengea na nikamuambia unaweza usione Simba kwa msimu ujao kwenye hatua ya makundi, kweli imetokea hivyo.

Unajua kwa nini nilisema vile? Nilisema vile kwa sababu mfumo wa Simba na timu kama AS Vita, Al Ahly, Mamelodi Sundown na TP Mazembe ni tofauti kabisa kama mbingu na ardhi.

Hapo kwenye mfumo ndio kwenye tatizo kubwa katika soka letu, yaani kila tukipapalika, tukifika hapo lazima tukwame.
Hadi sasa hata sijui klabu zetu na soka letu linaenda kwa mfumo gani, yaani tupotupo tu maana katikati hatupo na hata mbele na nyuma pia hatupo.

Tatizo la mfumo wa soka letu limeshikwa na wasaka tonge wengi ambao wao matumbo yao ni bora na wanayaheshimu kuliko kuendeleza mpira wenyewe.

Hii ni aibu kubwa huwezi kuingiza timu nne kwenye michuano ya Afrika na zote zisifike mbali na kama kweli TFF wako makini lazima hili jambo walijadili kwa kina na kuzihoji timu zote nne nini kimetokea.

Lazima timu hizo nne zijieleze zilikosea wapi au nini kilichangia zikwame maana tunapopata nafasi nne tukajua safari hii neema imeshuka kumbe majanga matupu.

TFF kazi kwenu kwenye hili lazima watu wajieleze ili safari nyingine tuweze kujua wapi pakuanzia maana hiyo ni aibu kwenye soka letu tunalopambana kulipandisha.

Hivi sasa Yanga baada ya kuondoshwa Ligi ya Mabingwa Afrika na kuangukia Kombe la Shirikisho Afrika, tuwaombee wafanye vizuri na kufika mbali.

Lakini katika kuwaombea huko, na wao wanatakiwa kubadilika, wacheze kwa kujituma, kama hawatabadilika, tusitegemee makubwa kutoka kwao.

2 COMMENTS:

  1. Ninachokiamini mimi lakini watanzania wengi au viongozi wengi wa mpira wanashindwa kupaangaza kwa jicho la shetani na naamini ndio tatizo letu kubwa linalotutesa si kwa vilabu au hata timu zetu za Taifa ni teuzi zetu za makocha.Inawezekana timu zetu zikawa zinaajiri makocha ambao hawana viwango vinavyostahili kuziandaa timu zetu kwenda kushindana na timu nyengine za Africa kwenye levo ya ubingwa wa Africa na kujikuta tukiangukia pua nakubaki kuwatupia lawama wachezaji.Au inawezekana pia ikawa timu zetu zinaajiri makocha wenye uwezo lakini makocha hao hawakai na timu zetu kwa kipindi stahiki cha kutengeneza mifumo yao na kuishia kufukuzwa au kocha kuondoka kutokana na timu zetu kushindwa kuwa na uwezo wa kumlipa stahiki zake kwa kushindwa kumugharamia.Mfano kama Lwandamina kipindi alipokuja kuifundisha Yanga angebakia mpaka sasa nadhani Yanga ingekuwa timu nyengine tofauti kabisa,hapana shaka wangekuwa wapo juu. Timu kama Azam wana uwezo kihali ila tatizo lao ile timu haijapata kocha anaestahiki labda tumtizame huyu mrundi atafanya nini.
    Simba wana uwezo sasa wa kihali ila kwa upande wa benchi lao la ufundi bado hawajapatia kwa asilimia zinazokizi shauku za watu wa Simba ya kuiona timu yao ikiwa na kiwango cha kujiamini cha kupambana na timu kama akina TP Mazembe nakadhalika. Ila nawapa saluti Simba ya sasa kutokana na ustahamilivu wanaonesha kwa kocha wao kwani yaliotokea kwa Simba klabu bingwa Africa mara hii ni suala la kocha kwa asilimia 100%. Nasema ni suala la kocha kwa sababu(1) kocha wa Simba ana maamuzi kwenye kikosi chake kwa asilimia mia moja. Hata baadhi ya wachezaji waliondoka Simba ilikuwa ni mapendekezo ya kocha licha ya baadhi ya wanasimba kuguna kwa kutokukubaliana na maamuzi ya kocha wao kuwaacha baadhi ya wachezaji fulani.Kocha hawezi kutoa mapendekezo ya mchezaji fulani aachwe kama hajampata mbadala wake la sivyo kocha huyo atakuwa ana namna.(2) Kocha wa Simba alipata muda kiasi wa kukaa na wachezaji wake kambini tena kambi yenye kukizi mahitaji yote. Kwangu mimi ninacho kiona tatizo kwa kocha wa Simba ni kocha mwenye kukosa kujiamini katika maamuzi na ndio maana licha ya baadhi ya wachezaji kucheza hovyo kule Msumbiji lakini bado kocha aliwang'ang'ania kuwachezesha wachezaji hao hao hapa Dar licha yakuwa Simba ilikuwa na rundo la wachezaji ambao pengine kama kocha angewaamini basi wangempa matokeo chanya. Niliiangalia mechi ya Simba kule Msumbiji yaani wale jamaa kama wangekuwa makini wangeimaliza Simba kulekule Msumbiji.Simba walicheza hovyo lakini cha kushangaza waliporejeana tena hapa Dar Simba haikuwa na mabadiliko yoyote ya maana na sikushangaa kabisa kuona Simba ikitupwa nje ya mashindano. Kwa kupitia ukurasa huu huu wa maoni baada ya mechi ya simba kule Msumbiji nilishauri viongozi wa Simba kufanya kikao na kocha wao kutokana na kiwango kibovu cha timu yao kule Msumbiji la sivyo wataishia raundi ya mwanzo na ndicho kilichotokea.Ni vizuri kuwapa makocha muda ila wakati mwengine kunahitaji moyo wa chuma na nadhani hii safari ya Mohamedi Mo ulaya sidhani kama akirudi huko atarudi peke yake?
    Kuhusu Yanga,watu wanatakiwa kuwa wastahamilivu kwani wamejitahidi vya kutosha. Wampe muda Zahera kwani hii timu alionayo ni mpya kabisa. Yaani Zahera anahitaji sapota ya hali ya juu bado apewe muda na hilo likifanyika basi Yanga watarajie makubwa. Zesco sio timu ya mchezo mchezo hata akina TP Mazembe wanachemsha pale. Nnaimani Zahera huyu huyu kama atapewa muda na usirikiano wa kutosha na timu yake hiihii basi mwakani hata aje Mazembe ataondoka tu.

    ReplyDelete
  2. Huu uandishi ninukanjanja ulioptiliza mwandishi anauliza maswali halafu huyo huyo ndio analazisha majibu yawe hivi basis wewe ulishindwaje kumuuliza demu wako auke wako nyumbani kuliko kuleta upuuzi wako hapa.
    Hebu tujifunze jambo moja wakati mashindano Hata yanapangwa ratiba iilikuwa nzuri ghafla Caf wakabadlilisha kwa hiyo kwa upande wa simba lilikuwa surprise kwao walichotegemea ikiwa kinyume ndio maana Hata simba daybilibidi wabadilishe kwa hiyo simba ilichemsha katika kuonfoa wachezaji wengi waliozoeana na kuingiza wachezaji wapya ambao walikuwa bdo kuzoeana pia Mpira ndivyo ulivyo matokeo waliopata simba ndio mpira ulivyo ukikosea unaadhibiwa ,kimbuka ud Songo ligibyao ilikuwa iko katikati ya msimu kwa hiyo timu ilikuwa vizuri tofauti na simba .
    Kwa upande wa Yanga pia bado sana timu yao bado ni ya kuunga unga angalia mattekeo waliyokuwa wanayapa katika mechi za kirafiki na timu walizokuws wanacheza Nazi ni za ajabu mno Yale sio maandalizi ya Caf champion league .

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic