MAAJABU YA MWANAMKE ALIYEZALIWA NA MIGUU MINNE
JOSEPHINE MYRTLE CORBIN, mrembo kutoka Jimbo la Texas, Marekani, alizaliwa siku ya Mei 12, 1868 akiwa na miguu minne.
Pamoja na kuzaliwa katika hali hiyo isiyo ya kawaida, madaktari walimchunguza na kumwona akiwa na afya na nguvu za kutosha kama binadamu wengine.
Kinyume na Afrika, Josephine angechukuliwa kama laana au janga na kuachwa msituni aliwe na wanyama, kwani katika watoto wenzake watano, ni yeye tu aliyekuwa na tofauti hiyo.
Pamoja na kuwa na miguu minne, alikuwa na sehemu mbili za via vya kike katikati ya kila pea ya miguu.
Akiwa na umri wa miaka 13, baba yake aliitumia fursa ya Josephine kuwa na tofauti hiyo, kwa kuwatoza watu hela waliotaka kumtazama alivyo; hivyo akawa anasafiri sehemu mbalimbali kufanya maonyesho ya viungo vyake hivyo.
Matokeo yake, aliweza kuingiza Sh. 46,000 kila wiki, kabla hajaamua kuolewa na Dk. Clinton Bicknell ambapo alipata ujauzito baadaye, ambao ulimletea matatizo makubwa kiasi cha madaktari kumshauri autoe ujauzito huo.
Hata hivyo, katika maisha yake alijifungua watoto wanne, ambapo ripoti zilisema alijifungua watoto hao kupitia katika via vyake viwili ambapo aliandelea kuishi maisha ya kawaida na familia yake.
Josephine aliishi kwa furaha na watoto na mumewe huko Texas hadi Mei 6, 1928, alipofariki kutokana na ugonjwa wa ngozi uitwao ‘streptococcal’ ambao leo hii unatibika kirahisi.
Familia yake walililinda kaburi lake la zege hadi ilipokauka ili kuzuia mwili wake kuchukuliwa na wataalam wa masuala ya tiba, wengi ambao walikuwa tayari kutoa fedha ili kuuchukua mwili huo wa Josephine Myrtle Corbin.
0 COMMENTS:
Post a Comment