October 28, 2019


Mbali na uwepo wa taarifa za uongozi wa Yanga kutaka kumrejesha kocha wake wa zamani, Hans van der Pluijm, kuna tetesi pia za aliyewahi kuwa kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen kupewa kazi.

Poulsen anatajwa kuchukua nafasi ya Mwinyi Zahera ambaye amekuwa hana matokeo mazuri ndani ya kikosi kwa siku za hivi karibuni.

Mbali na kuinoa Stars, Polsen pia aliwahi kuwa Mkurugenzi katika timu ya taifa ya vijana, Ngorongoro Heroes kabla ya kujiondoa kutokana na changamoto kadhaa kujitokeza.

Kwa tetesi zilizopo makocha wanaopewa nafasi kubwa ya kupewa mikataba Yanga endapo Zahera ataondoka ni Pluijm pamoja na Poulsen.

5 COMMENTS:

  1. Dah maisha ya soka yana changamoto hasa nikifikiria kocha papa Zahera alivyokuwa akiabudiwa kama mfalme Yanga.Hata hivyo namkubali sana Hans Plujim japo nasikia kuwa ana matatizo ya kubagua wachezaji.Kwa Kim itabidi Yanga isubiri sana kupata timu ya matokeo chanya kufuatana na falasafa yake.Nafikiri Yanga ingemvumilia kocha Zahera angalau akamalizia raundi ya ngwe ya kwanza ya ligi na kuangalia walichovuna.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kama mtu wa soka lazima uiangalie timu inavyopafom uwanjani. Timu ya Yanga ina mfumo wake. Winga mmoja na mido nyingi. Timu haifanyi vizuri kabisa

      Delete
  2. Watani Mbona Watawatimua Makocha Wengi Kwamfumo Watimu Yao

    ReplyDelete
  3. Watani kuweni wavumilivu mpaka round ya kwanza iishe na kubaliana na Anonymous

    ReplyDelete
  4. Kim Poulsen chaguo sahihi ni kocha mwenye mbinu za kisasa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic