October 9, 2019


Mke wa rapa T.I, Tameka Tiny Harris wikiendi hii ameibiwa vitu vyenye thamani ya bilioni 172 Pete ya ndoa, saa na heleni  ni vitu ambavyo mwanamke huyo ameibiwa ndani ya gari yake.

Mke wa T.I aliwaambia polisi kuwa, wizi huo ulitokea wakati yeye na rafiki yake walipokuwa wakipata kinywaji kwenye Baa moja mjini Atlanta, ambapo alirudi kwenye gari yake na kukuta vitu hivyo havipo.

Polisi wamedai hapakuwa na ishara yeyote ya gari ya mwanamma huyo kuvunjwa, lakini Tameka alisisitiza kupotelewa na begi iliyokuwa na vitu hivyo akiwa maeneo hayo

Upelelezi wa kumgundua mwizi unaendelea wakati ambao Tiny amegoma kuongea na mapaparazi juu ya ishu hiyo ambayo imeonekana kukosa ushahidi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic