October 30, 2019


IBRAHIM Akilimali, Katibu wa Baraza la Wazee la Klabu ya Yanga amesema kuwa bado anahitaji dua za watanzania kutokana na afya yake kutokuwa sawa kwani anasumbuliwa na maradhi.

Akizungumza na Championi Jumatano, Akilimali alisema kuwa anashukuru kwa sapoti anayopata kutoka kwa watanzania kutokana na mapito anayopitia anamini atarejea kwenye ubora wake.

“Kwa sasa bado afya yangu haijatengamaa nasumbuliwa na maradhi ya tumbo, imani yangu nitarejea kwenye ubora wangu kwani watanzania wapo pamoja nami wakiniombea dua.

“Kuhusu kudaiwa kwa sasa sina madeni nimekamilisha madai yote, ninachohitaji kwa sasa ni dua natarajia kurejea tena hospitali siku ya Alhamisi kwa kuwa ni siku ambayo nimeambiwa nirejee,” alisema Akilimali.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic