October 5, 2019


HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo FC amesema kuwa zile nane walizochapwa kwenye mchezo wa kirafiki mbele ya Azam FC hazitajiruida tena leo kwenye mchezo wa ligi licha ya kuwa wachezaji wake wengi wanasumbuliwa na majeruhi.

Namungo FC inacheza leo na Azam FC uwanja wa Azam Complex ina kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa kirafiki kwenye uwanja huo kwa kushushiwa kichapo cha mabao 8-1.

Akizungumza na Saleh Jembe, Thiery amesema kuwa wanaitambua Azam FC ubora wake ulipojificha kutokana na kupoteza mchezo wao wa kirafiki hivyo wataingia uwanjani kwa tahadhari.

“Ule ulikuwa ni mchezo wa kirafiki na ilikuwa haina maana kwamba tulitakiwa kufungwa mabao yale hapana ni wachezaji wenyewe kushindwa kutumia nafasi walizozipata.

“Kwa sasa tupo tayari ila nina wachezaji kadhaa ambao ni majeruhi ikiwa ni pamoja na Lusajo, Bigirimana Blaise,Paul Ngalema, Mo Ibra ” amesema Hitimana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic