POLISI TANZANIA YAKAMATA WACHEZAJI WANNE LIPULI, NONGA NDANI, WAPEWA KIPIGO
Wakati timu ya Lipuli ikitarajiwa kukipiga na Polisi Tanzania leo uongozi wa Lipuli unasikitika kuona Jeshi la Polisi limewakamata wachezaji wetu wanne.
Waliokamatwa ni Paul Nonga, Issa Ngoah, Seif Karihe na Daruwesh Saliboko na kuwapiga, kuwachania nguo na kuwapeleka kituo cha Polisi.
Tukio hilo limetokea leo majira ya saa moja jioni wakati wachezaji wetu kwa pamoja wakitoka katika ofisi za klabu zilizopo nje ya uwanja wa Samora.
Baadhi ya viongozi wa klabu wapo kituo cha Polisi kujaribu kufatilia kwa karibu jambo hili. Uongozi wa Lipuli unalaani vikali vitendo vyovyote ambavyo si vya kiungwana.
Imetolewa na Idara ya Habari na Mahusiano ya klabu ya Lipuli.
Ohh imekuwa hivyo tena.Wajomba mna matatizo gani tene??
ReplyDeleteNdio hivyo tena wajomba!!
ReplyDeletekwa hio kama wanashindwa kupata ushindi uwanjan,hio ndio wameona njia mmbadala,sasa soka letu linaelekea wapi
ReplyDeleteKabla ya kulaumu upande wowote ingekuwa vizuri kama tungejua sababu za kukamatwa hao wachezaji. Kama watakuwa walitenda kosa la jinai ni sahihi kukamatwa haitakuwa hujuma kinyume na hapo itakuwa sahihi kulaumu
ReplyDelete