October 11, 2019


OUSMANE Dembele nyota wa Barcelona ni rasmi ataukosa mchezo wa El Clasico dhidi ya Real Madrid kutokana na kufungiwa mechi mbili.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Octoba 26, na adhabu hiyo inatokana na kumtolea lugha chafu mwamuzi Antonio Miguel Mateu Lahoz.

Winga huyo alitolewa kwa kadi nyekundu wakati timu yake ilishinda mabao 4-0 dhidi ya Sevilla, wikiendi iliyopita.

Ripoti ya mwamuzi inaonesha kuwa Dembele mwenye miaka 22 alinukuliwa akitoa lugha hiyo Kali ndio maana akatolewa nje.

Atakosa mechi dhidi ya Eibar na Real Madrid kwani rufaa ya Barcelona ilipigwa chini mazima.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic