October 10, 2019


Ni kama hofu imetanda kwa mashabiki wengi wa Yanga kutokana na droo iliyofanyika usiku wa jana katika Kombe la Shirikisho Afrika.

Jana Yanga ilipangwa kucheza dhidi ya Pyramids FC ya Misri katika hatua ya Play-Off ili kufuzu kuingia hatua ya makundi ya mashindano hayo.

Baada ya droo hiyo, baadhi ya mashabiki wa Yanga wameonekana kuwa na uoga kutokana na takwimu za Pyramids ambayo imeshika nafasi ya pili kunako ligi hiyo.

Mbali na kuwa nafasi ya pili, timu hiyo pia imesajili wachezaji ghali zaidi ambapo baadhi yao wamegharimu kiasi cha zaidi ya bilioni moja.

Yanga itaanza safari yake hapa nyumbani kucheza na Pyramids Oktoba 27 kabla ya kwenda ugenini kurejeana nao Novemba 03 mwaka huu.


5 COMMENTS:

  1. chura kwa mwarabu hatoki hata awe mwarabu wa rufiji

    ReplyDelete
  2. Kandambili mwisho wenu hapo tunawasubiri kwa hamu safari hii mtapigwa wiki

    ReplyDelete
  3. Rudini muanze upya.Mpira hauchezwi kwenye midomo na magazeti.

    ReplyDelete
  4. Simba mnayo nafasi ya kuongelea mechi yenu na Yanga January hamna nafasi ya kuongelea mechi ya Yanga na Pyramids kwani kushinda au kushindwa kwa Yanga hakuwausu. Yenu yaliisha tangia mechi ya UD Songo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic