YANGA YASHTUKIA MSALA, KIKAO KIKAO CHAITISHWA, HUJUMA ZATAJWA
Mara baada ya kutoka sare ya mabao 3-3 na Polisi Tanzani, fasta uongozi wa Yanga, juzi usiku ulikutana kujadili mwenendo wa timu hiyo. Yanga walipata sare ya mabao 3-3 na Polisi Tanzania, mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Huo ulikuwa ni mchezo wa pili kwa Yanga tangu kuanza kwa Ligi Kuu Bara msimu huu, huku mmoja wakifungwa na Ruvu Shooting.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo Champini Jumamosi imezipata, mabosi wao walikutana kwenye moja ya hoteli jijini Dar na kujadiliana masuala mbalimbali ikiwemo ya matokeo ya michezo miwili ya ligi waliyoyapata.
Mtoa taarifa huyo alisema kikao hicho kiliongozwa na Makamu Mwenyekiti wa timu hiyo, Frederick Mwakalebela na Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, Rogers Gumbo kwa lengo la kuweka mikakati kabambe. Mtoa taarifa huyo alisema wanahisi hujuma kwa timu yao kutoka kwa watani wao.
Alisema kuwa, mikakati waliyoiweka ni kuhakikisha timu yao inapata ushindi katika michezo inayofuatia kwa kuanzia na Coastal Union watakaocheza kesho Jumapili.
“Kiukweli matokeo haya ya sare dhidi ya Polisi yametushtua kwani tulitarajia ushindi ambao ungeturudisha mchezoni baada ya matokeo ya Zesco lakini ikawa tofauti.
“Hivyo, uongozi ulikutana jana (juzi) usiku mara baada ya mchezo wetu wa ligi na Polisi kumalizika, hivyo tumeweka mikakati thabiti ya kupambana na hujuma za wapinzani wetu,” alisema mtoa taarifa huyo.
Alipotafutwa Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela kuzungumzia hilo alisema: “Kama uongozi hivi sasa tunatakiwa kuweka mikakati thabiti ya ushindi katika michezo yetu ijayo.
“Hivyo, kama uongozi tayari tumekutana kwa ajili ya kuweka mikakati ya ushindi, mashabiki watarajie furaha katika michezo ijayo kwa kuanzia mchezo wetu na Coastal.
Hebu nyie viongozi fikirieni kwanza kabla hamjataamka,mna ushahidi gani?walipeni stahiki za wachezaji kwa muda unaotakiwa halafu muone kazi.
ReplyDeleteOhh poleni sana watani mwaka huu sijui kama mtanusurika kushuka daraja
ReplyDeleteFukuzen kocha hafai kbsa
ReplyDeleteNilidhania Yanga wamepata viongozi wa mpira wasomi kumbe nimekosea kweli mpira wa sasa uanze kufikiria hujuma mbona mnafeli tafuteni matatzo ya team kitaalamu kwa kushirikisha technicals stuff ili wawaambie shida nn sio kukaa maboss wenye vitambi msio kuwa na utaalamu wa mpira mnaanza kuleta porojo za kwenye siasa hamuwezi kutibu ugonjwa mtaingia hasara kubwa jifunzeni ktk ulimwengu huu wa mpira leo hii kule manchester united inamaana maboss wakae kikao halafu watoke na jibu la hujuma kweli aaaah mwakalebala tuwe serious bhana.
ReplyDeleteNimepata taarifa kwamba viongozi wa Manchester United nao wamekaa kikao na kugundua kwamba wapinzani wao City nä Liverpool wanawafanyia hujuma.Kweli wajinga wengi sana Badala ya kutafuta kiini cha timu yetu kufanya vibaya wanataka kutuaminisha kwamba ni hujuma za Simba!!!Well well bwana kitambi ndio inaelekea mwisho wa uongozi wako.
ReplyDeleteSishangai kwani jana tu Mwenyekiti wetu Msola akihojiwa alisema "kuna wapuuzi wengi sana Yanga".Kweli mmetufanya wapuuzi tuamini upuuzi wenu.Kama klabu imewashinda mjiuzulu kuliko kuendeleza madudu.