October 8, 2019


Baada ya kukosa mechi za Ligi Kuu Bara msimu huu akiwa na kikosi cha Yanga, Kocha Mwinyi Zahera sasa amebakiza mechi moja pekee kuanza kukaa kwenye benchi la ufundi.

Hivi karibuni Kocha huyo ambaye ni raia wa Congo, alifungiwa mechi tatu baada ya kuingia uwanjani akiwa na mavazi ambayo si nadhifu huku kanuni za Bodi ya Ligi zikiwa haziruhusu.

Baada ya kifungo hicho, Zahera alikosa mechi mbili ambazo ni dhidi ya Polisi Tanzania na Coastal Union na sasa amebakiza mechi moja tu ili adhabu yake iishe.

Katika mechi mbili za Yanga zilizopita, bila Zahera, Yanga ilifanikiwa kupata alama nne baada ya sare ya 3-3 dhidi ya Polisi na ushindi wa bap 1-0 dhidi ya Coastal.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic