November 21, 2019


Kufuatia kuondoshwa kwa aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ambaye hivi sasa yuko kwao Congo, inaelezwa kuwa mabosi wa timu hiyo wanataka kumpa timu Charles Boniface Mkwasa.

Taarifa hizo zimekuja ikiwa ligi bado ipo raundi ya kwanza ya msimu katika ligi, ikitajwa kuwa mabosi hao hawana mpango wa kusajili Kocha mpya kutoka nje ya nchi kwa kipindi hiki.

Maamuzi hayo yankuja Yanga wakiwa na nia ya kuwajenga vizuri wachezaji wake kisaikolojia na kutovuruga zaidi mwenendo wa timu hivyo badala yake wanataka kuendelea na Mkwasa kwa msimu huu.

Mkwasa alichukua nafasi hiyo na ameingoza Yanga kucheza mechi moja ya ligi huku akishinda kwa bao 1-0 ikiwa ni dhidi ya Ndada huko Mtwara.

Kuna uwekezekano Yanga ikaanza kusaka Kocha mwingine mara baada ya msimu kumalizika ambaye anaweza akatokea nchi za Afrika Magharibi ama nje kabisa ya bara la Afrika.

6 COMMENTS:

  1. Mkwasa mbona yuko vizuri tu? Tatizo la wanayanga ni kutopenda kumpa mwalimu muda wa kutengeneza timu. Mijitu ya yanga yenyewe inapenda tu timu ishinde wakati mambo hayajakaa vizuri

    ReplyDelete
  2. WANAYANGA PATENI MAJIBU AMBAYO NI HAKI YENU KWA HAYA YAFUATAYO
    🔛Ningependa Kuwashauri Wanayanga Kuulizia Na Kufahamu Mambo Yafuatayo Ambayo Bado Yanautata....Ambayo Wengi Hawajapata Majibu Yanayoridhisha Na Yasipopatikana Yanaweza "Kuchafua Hali Ya Hewa" Pale Mtaa Wa Twiga & Jangwani.
    ⛔ Kocha Mkuu & Benchi La Ufundi Lililo Bora Na La Kisasa
    Baada Ya Kuondolewa Na Kuvunjiwa Mkataba Mwalimu Mwinyi Zahera Na Msaidizi Wake Noeli Mwandila Na Benchi Lote Ka Ufundi...Liliundwa Benchi La Muda Likiongozwa Na Charles Boniface Mkwassa Akisaidiana Na Saidi Maulidi SMG.....Hawa Waliambiwa Wanashikilia Timu Kwa Wiki 2 Wakati Ambapo Kocha Wa Kudumu Anatafutwa.
    Ukiangalia Ligi Kuu Ilivyo...Na Malengo Ya Klabu Kuchukua Ubingwa....Lazima Apatikane Kocha Mkuu Mwenye Kiwango Zaidi Ya Mkwassa Kwani Kulikuwa Hakuna Haja Ya Kumfukuza Zahera Ikiwa Hawakuweza Kumpata Mwalimu Mwenye Uwezo Wa Juu Zaidi Ya Mkwassa....Bado Ili Timu Ishindane Kwa Ubora Na Uimara Katika Kiuchezaji Na Timu Kama Simba Au Azam Lazima Kocha Wa Kudumu Awe Anatokea Katika Nchi Zilizo Na Uwezo Na Utaalamu Wa Kufundisha Soka Zaidi Ya Walimu Wanatokea Ukanda Huu Wa Afrika (Mashariki, Kati, Kusini Na Magharibi)
    ⛔ Ushauri Kuhusu Kocha
    Kocha Wanaotokea Serbia, Yugoslavia, Scotland, Amerika Kusini Ama Ulaya Magharibi Watafaa Kuifundisha Yanga Kwani Timu Inatakiwa Iimarike Kiuchezaji Na Kifalsafa
    ⛔ Kuacha Visingizio Vya Ukosefu Wa Pesa
    Kuna Dhana Inayojengeka Kuwa Timu Haina Fedha Kwa Hiyo Tuiishie Kufundishwa Na Wazawa Ambao Uwezo Wao Ni Wa Kawaida Hii Ni Dhana Potofu Ambayo Haina Ukweli Wowote. Yanga Ni Timu Kubwa Ambayo Ina Udhamini Wa Makampuni Zaidi Ya 4 (SportPesa, Taifa Gas, GSM, Maji Ya Afya, Azam Media) Pamoja Na Vodacom....Pili Yanga Ina Wanachama Na Mashabiki Wenye Uwezo Mkubwa Wa Kifedha Wanaojitolea Kuilipia Gharama Kubwa Kubwa Mifano Mingi Ipo Kudhihirisha Hili Kama Ambavyo Ilivyofanyika Huko Nyuma. Isitoshe, Kuendana Na Ukubwa Wa Jina La Yanga Na Msukumo Unaotokana Na Uwekezaji Uliofanyika Simba Itakuwa Ni Aibu Kwa Yanga Kutoingia Kwenye Mabadiliko Ya Kiundeshaji Na Kupata Mwekezaji Ama Wawekezaji/ Ambao Wana Uwezo Kuzidi Hata Huyo Aliyepo Simba...
    ⛔ Uwanja Wa Kaunda Na Kigamboni
    Kumekuwa Na Kusuasua Na Mwendo Wa Kinyonga Katika Utekelezaji Wa Ukarabati Na Ujenzi Wa Uwanja Wa Mazoezi Wa Yanga. Wapenzi Na Mashabiki Wanahoji Hili Na Hasa Wanapoona Wenzao Mtaa Wa Pili Wao Wamekamilisha Uwanja Wao...Ila Yanga Zimebaki Porojo Na Siasa Tu....ILI LAZIMA LIISHE WANAYANGA WAMECHOKA WANATAKA VITENDO

    🚫 Maswali
    ✔ Kwanini Kuna Kusuasua Na Kujivutavuta Kuingia Katika Uwekezaji Na Mabadiliko Katika Yanga Huku Kukiwa Na Kushindwa Kwa Kamati Lukuki Zilizoteuliwa Kuleta Mabadiliko Au Kufanya Vitendo Vinavyoonekana?
    ✔ Je, Viongozi Wana Nia Ya Dhati Ya Kuiinua Yanga Kiuchumi? Kama Wanayo Mbona Mchakato Wa Mabadiliko Unachelewa?
    ✔ Je, Kama Hauchelewi Na Kama Haurakishwi Kwanini Kuna Kilio Cha Ukata Wa Fedha Na Kutaka "KUENDESHA MAMBO KIZAMANI KWA MFUMO WA KARNE YA 19 WAKATI TUPO KARNE YA 21???? Mpira Ni Pesa Na Matokeo Mazuri Na Uendeshaji Wa Timu Kwamaana Ya Benchi La Bora La Ufundi, Miundo Mbinu Bora, Kambi Na Huduma Za Wachezaji Bora Hutokana Na Uwekezaji Wa Pesa....Kwani Uongozi Uliochaguliwa Ulisema Ndani Ya Miezi 3 Hadi 6 Wataiingiza Yanga Katika Mabadiliko Hili Mbona Unasuasua???

    🚫 Wenu Katika Kutoa Ushauri Chanya Kwa Ajili Ya Maendeleo Ya Mpira Tanzania!

    Ahsanteni

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tumeweka imani na fikra zetu za kufundishwa ma walimu kutoka nje ndio uimara wa timu. Tunachokosa kwenye timu zetu ni uwekezaji wenye tija katika kuendesha mfumo mzima wa mpira wetu. Makocha wetu wapo vizuri sana ila wanapata shida pale kwenye utimiziwaji wa mambo ya timu punde wanapohitaji. Kocha mzawa atalipwa mshahara mdogo, timu haiwezi kuweka kambi nje ya nchi hata kama atasema, vifaa vya michezo vitakuwa duni na mambo mengine mengi. Tatizo "huyu ni mtanzania anajua mfumo wa nchi yetu.

      Akija mgeni viongozi wataogopa kuaibika watatimiza kila atakalo mwalimu. Timu itakwenda uturuki au Afrika Kusini, itakaa hotel nzuri na mambo mengine. Tatizo si akina Mkwasa kupewa timu..tatizo ni viongozi kumuwezesha huyu mzawa kwenye kila hitaji. Angalia Kocha Katwila pale Mtibwa...akila Mecky Mexime pale Kagera...wakipewa kila hitaji..timu zao zitakuwa imara zaidi. Mecky hawezi kusema anataka mchezaji wa nje..ataulizwa malengo yao si kuchukua ubingwa ila ni kubaki ligi kuu.

      Wachezaji kumuamini kocha mzawa pia ni tatizo..wanatakiwa kujua thamani ya kocha anaeletwa...

      Kwenye suala la fedha...hilo ngoja tuwaachie wenyewe..wakifikia muafaka watatoa majibu...maana Siri ya Mtungi aijuae kata

      Delete
    2. Sikatai uwezo wa makocha wazawa ila wanapungukiwa na Mbinu na kujiongeza katika falsafa mpya za soka la kisasa na mabadiliko yanayofanyika duniani katika taaluma yao ya Ukocha...hapo ndipo wanapozidiwa, wangekuwa wamejiongeza kielimu na kimasomo hili lisingezua mjadala lakini tafiti nyingi na Uzoefu unaonyesha mapungufu hayo na ndio maana klabu zinatafuta makocha wanaotoka nje ambao wamewazidi wazawa katika mbinu za kisasa na katika falsafa mpya ya soka inayobadilika haraka katika karne ya 21

      Delete
  3. Umenena ndugu ni kweli makocha wazawa hawaendi na muda. Kwanini hasa uwezi kusikia kocha toka tz akifundisha soka nje ya nchi?,Tunazidiwa hata na Burundi makocha wetu vilaza kujiongeza hakuna halafu ni wakosoaji.Sasa huyo Mkwawa ana mbinu ipi Yanga mmechemsha semeni Zahera mlishindwa kumlipa kwani hata sababu za kumfukuza haziingii akilini.Nyie Yanga mlijua kama mngecheza mechi za kimataifa so mliokota tu dodo limedondoka.Kwahiyo kumlaumu Mwinyi kwa matokeo ya mechi zile hamkumtendea hali mngemlaumu kwenye ligi.Mpeni Mkwasa basi ule mishahara wa Zahera kama kweli mna fedha acheni hizo muwe wa kweli.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic