November 24, 2019


Watu zaidi ya 36 wamefariki dunia baada ya maporomoko ya udongo kutokea eneo la Pokot Magharibi mwa nchi ya Kenya.

Vifo hivyo vimetokea baada ya nyumba zao kusombwa na mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika eneo hilo.

Maporomoko hayo yameathiri zaidi vijiji vya Nyarkulian na Parua, ambavyo vinasemekana kutenganishwa baada ya daraja kusombwa na mafuriko. Maafisa pia wamesema kuwa miili ya watu 12, ikiwemo ya watoto saba imepatikana.

Joel Bulal, mmoja wa wasimamizi wa serikali katika eneo hilo amesema kuwa shughuli za uokozi zinaenedelea.

Kamishina wa jimbo hilo, Apollo Okelo amesema watu wengine wengi huenda wamekwama chini ya matope na kuongeza kuwa shughuli ya kuwaokoa zinaathiriwana hali mbaya ya hewa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic