November 24, 2019


Kocha wa Paris Saint- Germain, Thomas Tuchel hakuwa tayari kung’ata maneno kuhusu kitendo cha nyota wa timu yake, Neymar kusafiri kutoka Ufaransa kwenda Madrid licha ya kuwa ni majeruhi.

Neymar alisafiri kwenda Madrid kuangalia mchezo wa tenisi katika Davis Cup licha ya kuwa alikuwa majeruhi na alitakiwa kupumzika kuelekea kurejea uwanjani hivi karibuni.

Alitarajiwa kurejea uwanjani jana katika mechi dhidi ya Lille, huku timu yake pia ikiwa kwenye maadalizi ya kujiandaa na mchezo mgumu dhidi ya Real Madrid, Jumanne ijayo.

“Unataka nifanye nini?” alilalama Tuchel na kuendelea: “Mimi siyo baba yake, wala siyo polisi, mimi ni kocha wake tu.

“Nikiwa kama kocha ni wazi sipendi hali kama hiyo, lakini siwezi kupoteza utulivu wangu wa akili kuhusu hilo. Ni (Nyemar) mchezaji wa kulipwa na anajitambua, amekuwa akifanya mazoezi vizuri zaidi ya wenzake ndani ya wiki mbili zilizopita.”

PSG ilitarajiwa kuwakosa Marco Verratti na Ander Herrera katika mchezo huo wakati Kylian Mbappe alikuwa akisumbuliwa na homa hadi juzi jioni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic