Heshima yangu, kama nilivyoumbwa si ya kujivuna, ni kuheshimu kila mtu na hali yake, masikini au tajiri, ndivyo nilivyoumbwa.
Kudamshi mie sikusubiri niwe msemaji, nitakuwa mpuuzi nikianza kutangaza kwa umma kwamba, navaa vizuri naenda kujirusha, kwa mwenye akili, mwenye familia, anayeijali hawezi kutamba kwa hilo.
Simu ni kitu gani, mawasiliano tu brother, simu zangu ni ndogo kiumbo lkn ni kubwa kiuwezo, na ukiona mtu anajitapa kwamba anachokitu fulani ambacho fulani hana, mchunguze vizuri, hayuko sawa huyo. Mimi siyo limbukeni, niko vizuri.
Uswekeni sitaki hata kulizungumzia, lakini maisha yangu yako poa, naitunza familia, inaishi vizuri, hatuna shida kwa kweli.
Sijui kujirusha, ili iweje?
Tangu nizaliwe sijawahi kuonja harufu ya pombe, wala kwenda disco, hata soda sinywi, na huo ushatani mwingine kwangu mwiko kabisa, naishi maisha ya kumfurahisha Mungu pamoja na wanadamu wenye akili tu...
Mimi nazungumzia mpira, sikuajiriwa Ruvu Shooting kuzungumzia watu na maisha yao, wala kujivuna kwamba nina hiki, ambacho fulani hana!
Nisameheni katika majibizano ya kutafuta kuonekana mimi ni bora kuliko wengine, ninavyo wasivyonavyo, siyo tabia yangu.
Karibuni Mabatini, tufurahi pamoja.
Mungu wetu ni mwema.
Na Masau Bwire, Msemaji wa Ruvu Shooting
safi kabsa braza masau msamehe tu huyo mana hajtambui na hayuko sawa kikfkra kla mtu anajua endelea kuwaadabsha hao watu wasiosoma mana na huyo ni mbumbumbu kama mambumbumbu wengine.
ReplyDeleteManara anamapungufu makubwa sana kuhusu neema finyu alizojaaliwa ba Mungu. Kuna muda anajitoaga ufahamu kabisa na kuzungumza mambo ya kipuuzi. Usemaji wa timu yake anautumia hata kuwaona wengine wapuuzi na hakuna wanalolifanya.
ReplyDeleteNimemuona Masau Bwire kamjibu kwa hekima kubwa sana na kuonyesha yeye ni mkongwe kiasi gani katika usemaji wa timu. Mungu Akujalie zaidi msemaji wa Ruvu Shooting na Heshima yako ibaki na izidi kusambaa na kwa wasemaji wa timu zingine wenye maneno mabaya kama msemaji wa Simba
Mimi ni shabiki wa Simba, lakini kwa message hii Masau yupo sahihi kabisa. Anaonyesha ni jinsi gani amekomaa kielimu na pia ana hofu na Mungu wake.
ReplyDeleteMasau umemrudisha mtu darasani!! kama ni muelewa atakua kapata somo la kutosha
ReplyDeleteUkiwa muongo usiwe msahaulifu.Misimu miwili iliyopita Kadai Bwire alifungua utani na Simba.Alinunua kinyango mfano wa Simba akapiga picha kwamba watampakata Simba kwani ni Simba wa Kariakoo.Anadai timu yake inapapasa watu.Kupapasa ni neno sahihi kutumika kwenye mpira?Ukianza utani usichague mipaka!Haji Manara ametania Masau Bwire kadai amenyanyaswa!Usitupe mawe kwenye nyumba ya vioo nä wewe unaishi kwenye nyumba ya vioo.Au kwa ustaarabu wa Masau Bwire wanaume wanapapaswa ?Kama huwezi joto la jikoni basi usiingie jikoni.
ReplyDeleteMasau bwire ulibanwa mbavu km ulsema unataka kupapasa simba vipi Leo?
ReplyDeleteMimi ni mkereketwa wa Simba, na clip ya Manara ninayo. Ila maneno ya Manara hayakuwa na utani wa soka ila yalikuwa binasfi. Masau Bwire aalizungumzia kuipapasa timu hakumtaja Manara. Tukubali msemaji wetu aliteleza na Bwire katumia busara kujibu.
ReplyDeleteProtas-Iringa