November 24, 2019


KOCHA mpya wa Tottenham, Jose Mourinho amefichua kuwa mabosi wa klabu yake ya zamani, Manchester United wamempigia simu kumpongeza na kumtakia kila la kheri katika majukumu yake mapya.

Mtendaji Mkuu wa Man United, Ed Woodward ni mmoja wa mabosi hao waliohusika kumpigia simu Mreno huyo mara baada ya kutangazwa kuwa kocha mpya wa Tottenham.

Mourinho alifukuzwa kazi na Woodward miezi 11 iliyopita kutokana na matokeo mabaya na kushindwa kuelewana na wachezaji wa timu hiyo ya mitaa ya Old Trafford.

Akizungumzia suala hilo, Mourinho alisema: “Labda niombe radhi kwa kutopokea simu zaidi ya 500 kwa kuwa kwa jumla nilipigiwa simu 700 lakini nikafanikiwa kupokea 200 kati ya hizo.

“Lilikuwa jambo zuri kuona napata pongezi kutoka kwa klabu yangu ya zamani, watu wengi wamenionyesha heshima, ni jambo zuri na limenigusa sana.

“Wote walikuwa ni watu muhimu kwangu, nilipigiwa na Richard Arnold (mkurugenzi wa michezo wa United), wa tatu au wanne hivi alikuwa Ed Woodward, wote hao walikuwa ni mabosi wangu.”

Kupewa posho

Wakati huohuo, kocha huyo anatarajiwa kupata nyongeza ya pauni milioni 2 (Sh bilioni 5) katika mshahara wake mwishoni mwa msimu huu ikiwa atafanikiwa kuiwezesha kushika nafasi nne za juu katika Premier League.

“Nikiwa kama kocha ni wazi sipendi hali kama hiyo, lakini siwezi kupoteza utulivu…

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic