November 24, 2019


Licha ya kupapaswa kwa jumla ya mabao 3-0 dhidi ya Simba, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amewaponda wapinzani wake.

Masau amesema kuwa Simba hawakucheza mchezo mzuri na hata mabao yao yalikuwa hayana mipango.

Ikumbukwe Masau awali alitamba kuwa jana ingekuwa zamu ya Simba kula kichapo baada ya kuzifunga timu za Azam FC, Yanga na KMC.

Ushindi huo ulizidi kuwafanya Simba warejee kileleni kwa kufikisha jumla ya alama 25 ikiwa imecheza mechi 10.

"Hakuna mpira wa maana walioucheza Simba, mabao yao yalikuwa hayana mipango, yalikuwa mepesi mno, tofauti na sisi tuliocheza soka safi," amesema Masau.

3 COMMENTS:

  1. Kweli unayoyasemam kuwa mchezo haukuwa wa mana kwani magoli matatu yalikuwa kidogo mno na umesahau kuwa kutokana na hesabu za wadadisi ni bora ukumbushwe kuwa timu yako imefungwa na mnyamama mara nane mfululizo bila ya rehema na kwakuwa mliifunga Yanga ukahisi mnyama atakuwa mboga na matokeo ya Jana ambayo hukuyategemea ndio yakakufanya unatoa kauli zisizo na mizani

    ReplyDelete
  2. Pole sana Brother Masawe,mimi ninakukubali sana lakini jana umepapaswa na makucha ya mnyama.Tafadhali jihadhari na mnyama hana masihara akiona nyama tamu

    ReplyDelete
  3. Hatutaki porojo almuiimu mumechapwa tatu. Iyoneeni Yanga lakini Simba mwiko

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic