November 24, 2019


PICHA limekwisha! Rasmi leo Kocha Mkuu wa Simba Mbelgiji, Patrick Aussems kuna uwezekano mkubwa kakaondoka ndani ya klabu hiyo baada ya mchezo wa jana dhidi ya Ruvu Shooting.

Kocha huyo hivi karibuni aliondoka nchini ghafla huku akiomba ruhusa kwa mabosi wake ikiwa ni saa chache kabla ya kusafiri ikielezwa kwenda kufanya mazungumzo na klabu ya Polokwane FC ya nchini Afrika Kusini atakayokwenda kuifundisha.

Wakati kocha huyo akiwa nchini huko taarifa zilienea lakini Simba tayari walikuwa wakifanya mazungumzo na Kocha wao wa zamani, Mserbia Goran Kopunovic.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumamosi, kocha huyo juzi usiku alikutana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa na kufanya kikao kizito ambacho kilifikia muafaka mzuri wa pande zote mbili katika kusitisha mkataba.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa katika kikao hicho wamefikiana makubaliano ya kumalizia mchezo wa mwisho wa ligi kabla ya kusimama unaotarajiwa kupigwa leo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam watakapocheza na Ruvu.

Aliongeza kuwa ilitakiwa kocha huyo atangazwe tangu juzi lakini mchezo wa Ruvu ndiyo umevuruga mipango hiyo na walifikia kuchukua maamuzi hayo kwa kuhofia kuwavuruga kisaikolojia wachezaji watakapokuwa uwanjani.

“Ilikuwa ni ngumu kutangaza kuachana na kocha juzi Jumatano wakati tukiwa tunajiandaa na mchezo mgumu dhidi ya Ruvu, lakini ukweli ni kwamba mchezo wetu wa ligi wa kesho (jana) utakuwa wa mwisho kwake kukaa benchi yeye pamoja na benchi zima la ufundi.

“Kikubwa viongozi walikuwa wanahofia kutangaza kuachana na yeye kwa sababu ya kuwachanganya kisaikolojia wachezaji wetu tukielekea katika mchezo huo, hivyo kama viongozi wameona umuhimu wa mchezo huo kwa kumpa mechi ya mwisho yeye pamoja na benchi la ufundi kukaa kwa mara ya mwisho kabla ya kulivunja benchi.

“Hayo yote yalifikiwa muafaka baada ya kikao kizito kilichofanyika juzi usiku kati ya kocha huyo na mtendaji wetu mpya, hivyo Aussems atautumia mchezo kama sehemu ya kuwaaga wachezaji na mashabiki wa timu hiyo atakapokaa benchi,” alisema mtoa taarifa huyo.

Aussems alizungumzia hilo mara baada ya mazoezi ya mwisho yaliyofanyika jana asubuhi kwenye Uwanja Gymkhana jijini Dar es Salaam na kusema kuwa: “Niwaondoe hofu mashabiki kuwa mimi bado kocha wa Simba na waachane na tetesi hizo zinazoendelea za mimi kufukuzwa, kikubwa wao wajitokeza uwanjani kuisapoti timu yao itakapokuwa ikicheza na Ruvu.”

Naye mtendaji wa timu hiyo, Senzo alisema kuwa: “Aussems bado kocha wa Simba, hizo taarifa siyo rasmi za kuachana na kocha wetu na nisingependa kuzungumzia hilo, hivi sasa akili zetu zote tumezielekeza kwenye mchezo wetu wa ligi dhidi ya Ruvu.”

Katika hatua nyingine, gazeti hili limepata taarifa za Bodi ya Utendaji ya timu hiyo kupitia baadhi ya makocha wanaotarajiwa kumrithi Aussems anayetarajiwa kuondoka wakati wowote nchini ikielezwa kuelekea Polokwane.

Habari za ndani zinadai kwamba Aussems ameshamalizana na Polokwane na anatakiwa kuwa kwenye benchi Jumanne dhidi ya Orlando Pirates kwani tayari aliyekuwa Kocha Mkuu ameshapigwa chini.

Kwa mujibu wa Gazeti la Soccer Laduma la Afrika Kusini, mechi dhidi ya Orlando ni ngumu kwa Polokwane na wanataka benchi pawe na Kocha mpya.

CHANZO: CHAMPIONI

7 COMMENTS:

  1. Kama hali iko hiyo viongozi wa simba Ni bure kabisa mm binafsi sioni sababu ya kubadili kocha,acheni kufuata mkumbo wa yanga

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nilivyoelewa mimi ni kuwa kocha Aussems ameamua kuvunja mkataba hivyo ni yeye anayetaka kcha anataka kuachana na Simba.Utamlazimisha?

      Delete
  2. Ndugu yangu inaonekana kilichoongelewa hapa hujakielewa, sasa wasiachane na kocha wakati kocha mwenyewe ndo anaetaka kuondoka? Kocha amepata dili la pesa ndefu kuliko anachokipata hapo hivyo yy ndo anaetaka kuondoka na yy ndo anaevunja mkataba, simba ni lazima wamruhusu baada ya makubaliano ya kuuvunja mkataba wake

    ReplyDelete
  3. Ila kwa maelezo ya kocha mwenyewe, inaonekana alitafuta timu baada ya kuona dalili mbaya za simba za kutaka kumuondoa, sasa haieleweki

    ReplyDelete
  4. Ila ukimckiliza kocha mwenyewe unaweza ukawa uko sawa coz kocha analalamikia maamuzi ya simba kuvunja nae mkataba

    ReplyDelete
  5. halafu baadaye mnamrudisha kama mnavyotaka kufanya kwa makocha waliopita

    ReplyDelete
  6. Navyohisi mimi kocha Aussems amekuwa hana wakati mzuri tokea Simba itolewe mapema raundi ya kwanza ya klabu bingwa ya Africa bila kutarajiwa na UD Song na pengine hili limemtoa kwenye reli na kumuadhiri kisakolojia.
    Mie binafsi nahisi sio kocha tu pia hata benchi zima la ufundi na wachezaji hawana morali kama walikuwa nayo msimu uliopita.Hapa viongozi walitakiwa kutafuta wataalamu wa saikolojia kuwarejesha kocha, benchi la ufundi na wachezaji ktk uhalisia wao waliokuwa nao msimu uliopita.Kumbukeni mechi walizocheza wakati wa Simba day na Ngao ya jamii na hata ya UD Songo dsm jinsi timu ilivyocheza kwa ari na juhudi na soka iliyoeleweka.Baada ya michezo hiyo sioni tena kama Simba inacheza soka la kujituma.Perfomance, tactical technique na pia hata ukirejea kwenye takwimu ya football possesion ya mechi walizocheza ni dhahiri imepungua sana.Pengine Kocha Aussems na viongozi wameshaliona hilo hivyo pande mbili kwa maana ya kocha na viongozi wamekaa na ku jadili mwenendo wa timu na malengo yanayokusudiwa kama kuna mwelekeo chanya au hasi? Pengine wameona ni bora kuachana kwa amani na maisha yaendelee.Sisi mashabiki tusiwe na hulka ya kuhukumu haraka bila ya kuangalia upande wa pili wa shilingi.Je kama kocha Aussems ndio aliyeamua kuvunja mkataba kwa maslahi yake binafsi, sie ni nani tumlazimishe aendelee kubaki?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic