MIKEL Arteta, Kocha Mkuu wa Arsenal amepanga kuboresha kikosi chake kwenye dirisha la usajili wa mwezi Januari, 2020 kwa kumvutia kasi beki wa RB Leipzig, Dayot Upamecano.
Imeripotiwa kuwa Arsenal ipo tayari kutoa dau lolote ambalo mabosi wa Upamecano watahitaji ili kumpata beki huyo ambaye ni pendekezo la Arteta.
Kwenye jumla ya mechi 20 za Ligi Kuu England msimu huu, Arsenal imefungwa jumla ya mabao 31 jambo linalompasua kichwa bosi huyo mpya.
Arteta amesema kuwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Chelsea wakiwa nyumbani haimanishi hawana uwezo bado wana nafasi ya kuimarisha kikosi chao.
Inatajwa kuwa dau la kumpata nyota huyo ni pauni milioni 50 na tayari Kocha wa Spurs Jose Mourinho naye ameonyesha dalili za kuipata saini ya beki huyo.
Mabao ya ushindi kwa Chelsea yalifungwa na Jorginho pamoja na Abraham huku lile la Arsenal likifungwa na Pierre Aubameyang.
0 COMMENTS:
Post a Comment