December 25, 2019


KIUNGO wa timu ya Leicester City, Wilfred Ndidi ameingia kwenye anga za kuwindwa na bosi mpya wa Arsenal, Mikel Arteta.
Arteta amepewa mkataba wa miaka mitatu na nusu kuinoa timu hiyo ya Arsenal akichukua mikoba ya Unai Emery ambaye alipigwa chini inaelezwa kuwa amependekeza jina la Ndidi kusajiliwa kwenye dirisha la mwezi Januari,2020.
Inaelezwa kuwa Arsenal imetenga kiasi cha pauni milioni 40 ili kuipata saini ya nyota huyo ambaye amekuwa bora ndani ya kikosi chake cha Leicester City kwa sasa.

Ndidi anatajwa kwenda kuchukua nafasi ya Granit Xhaka ambaye amekuwa hana nafasi ndani ya kikosi hicho  baada ya kuzinguana na mashabiki na alivuliwa kitambaa cha unahodha ambacho kipo mikononi mwa Pierre Aubameyang.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic