HAPA NDIPO MONDI ANAPOWAPOTEZA WENGI
Staili yake ya maisha, mafanikio na ushawishi, mwanamuziki kinara wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ni bingwa katika kiwanda cha burudani.
Kwa furaha ya kuwa na mashabiki wengi hasa warembo, Diamond au Mondi ameyafanya maisha yake kuwa sehemu ya kumsaidia jina lake kuwa imara zaidi masikioni mwa watu na kukamata hisia za wengi.
Mondi ni bingwa wa skendo. Ni bingwa wa ushindi katika mabifu na wenzake.
SKENDO
Angalia skendo zake tangu awali. Tangu kipindi kile anatoka kima-penzi na yule Miss Kiswahili, Rehema Fabian hadi sasa akiwa na Tanasha Donna. Kote huko utagundua kuwa mahusiano yake mengi ya kimapenzi yalimfanya si tu kuzungumzwa, ila kujitengenezea jina na mkwanja zaidi.
Mastaa wengine wanaotamani kuwa kariba yake, wakizama mapenzini hupoteza kabisa malengo kwenye kazi. Kwa Mondi, yeye hutumia mahusiano yake kumtangaza na kumuo-ngezea mashabiki.
Mfano rahisi ni uhusiano wake na mwigizaji Wema Isaac Sepetu. Wakati Mondi anatoka na Wema, ilionekana kama mrembo huyo ‘anamsaidia’ kupanda, lakini mara tu walipoachana ikaonekana Wema anapoteza almasi baharini.
Hii inata-fsiri kuwa wakati We-ma ana-kuwa na Mo-ndi, Wema alikuwa kwenye kilele chake cha umaarufu, lakini wakati anaachana na Wema, Mondi alikuwa juu zaidi ya Wema. Hii maana yake nini?
Katika kipindi cha uhusiano wake na Wema, mbali na skendo na vituko vingi ikiwemo kuvishana pete, Mondi alikuwa akiendelea kupambana, kujisogeza matawi ya juu huku Wema akiwa palepale, akila raha za umaarufu.
MABIFU
Achana na suala la kuwa na warembo kibao, mtazame Mondi kwenye mabifu. Muweke kando kwanza Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’, tujadili kidogo wengine.
Wakati f’lani Mondi akiwa na ukaribu na Shetta, jina la msanii huyo lilikuwa juu na kila mmoja alikuwa akiinjoi kazi zake. Angalia kilichotokea, baada ya kudaiwa kuwa kwenye uhasama. Jina la Shetta siyo tu lilififia ila hata zile kolabo kalikali alizokuwa akifanya na wanamuziki wengi wa nje ya Bongo, zilitoweka.
Hicho ndicho kinachosemekana kuwakumba Dimpoz na Nay. Kuna kitu kimoja maalum sana kuhusu Mondi.
Akiwa na furaha, ataachia ngoma za kufurahi na kupiga pesa. Akiwa katika simanzi na ukiwa, ataachia ngoma za namna hiyo na kutengeneza utajiri.
Mondi anasema Ngoma ya Mawazo aliitunga baada ya kuumizwa na kuachana na Wema. Kwa watu wengi hiki siyo kitu cha kawaida.
Mara nyingi wengi wakiwa na huzuni, hushindwa kutumia nguvu iliyojificha kwenye huzuni zao kufanya mambo makubwa. Lakini Mondi kazi hiyo anaiweza na inampa mafanikio na hapo ndipo anapowapoteza wengine.
Wakati akielekea kwenye kilele cha tamasha lake la Wasafi, Mondi akaachia Ngoma ya Baba Lao. Ngoma f’lani hivi ya kawaida ila ina vaibu la kutosha. Angalia watu walivyoruka nalo na linavyoendelea kutesa mtaani.
Wengi wanashindwa kumtazama Mondi kwenye picha yake halisi. Wasanii wengi hukimbilia kumtazama Mondi kwenye eneo la mapenzi na skendo bila kujua hasa kinachomjenga zaidi ni kazi huku skendo na vituko vyake vikitumika kumtangaza.
Mondi anajitangaza kwa fujo. Uhusiano wake na Zari siyo tu ulikuwa na habari nyingi, ila pia alitumia akili na umaarufu wa mwanamke huyo kumfanya azidi kuwa lulu machoni kwa wengi. Jambo hili limewashinda mastaa wengi. Limemshinda Ben Pol, Jux, Dimpoz, Shetta na hata Nay alijaribu mwanzoni, lakini ikashindikana.
Hebu muone Ben Pol, anazunguka tu duniani akiwa na mpenzi wake yule bilionea wa Kenya, Anerlisa. Baada ya kuwa na bilionea huyo, Ben Pol amefanya nini kikubwa kwenye muziki wake? Hakuna. Sanaa yake imepanda thamani kwa kiwango gani baada ya uhusiano huo? Hakuna jibu. Kuhusu resi zake na Kiba na Harmonize, tuweke nukta kidogo, muda utasema!
Baada ya kilichotokea kwa mwigizaji Yusuf Mlela na mchekeshaji Ebitoke, nikamkumbuka sana Mondi. Mlela ni miongoni mwa waigizaji wa Bongo Muvi aliyeaminika atakuja kuwa staa mkubwa sana baada ya kina Kanumba na Ray, lakini hadi sasa hakuna kitu.
Mlela, pamoja na kujua kuigiza na kuwa na mashabiki wengi, lakini hana ubunifu wa maana wa kumfikisha mbali. Bila shaka naye anawaza kama wenzake wanavyowaza. Kwamba kwa wingi wa skendo na vituko, watakuwa maarufu zaidi na kupata mashabiki wengi.
Skendo ni kama nazi tu kwenye maharage, kama mtu akifanya kwa ‘timing’. Nazi isipokuwepo kwenye maharage, mlaji hawezi kulalamika ila ikiweka vizuri, mlaji anaweza asimsahau mpishi wa maharage hayo.
Skendo haina maana kama mhusika hana kazi ya maana sokoni. Fanya utafiti kuangalia umaarufu wa Wema sasa. Hata kwa bahati mbaya, hawezi kuwa kama alivyokuwa zamani. Kipindi kile ungeona skendo yake leo kisha kesho ungekutana na filamu kali aliyoigiza. Siku hizi yupo tu, siyo kama zamani.
Mlela na Hemed PHD ni miongoni mwa silaha ambazo tuliamini zingekuja kuleta mageuzi katika kizazi kipya cha filamu, ila wamelala. Wakihojiwa ni kulamba midomo na kujisifia sura na kupendwa na mabinti. Katika hali kama hii, mawazo kama haya unadhani nini kinatokea?
Akina Mlela wangejua thamani na wajibu wao kwenye soko la filamu, wala soko hilo lisingepoteza msisimko. Wapenzi wa filamu siyo kwamba hawapo, wapo wengi pengine kuliko ilivyowahi kuwa, ila hawapati filamu za maana ndiyo maana wanakimbilia kwenye filamu za Kikorea na Kifilipino.
0 COMMENTS:
Post a Comment