TIMU zote Bongo zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa ni pamoja na Lipuli, Singida United, Mbeya City, Simba, Kagera Sugar, Yanga, Azam FC zimepewa angalizo kali endapo zitashindwa kufanya usajili kwa wakati.
Kupitia taarifa rasmi iliyotolewa na Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Cliford Ndimbo, imezitaka timu hizo kukamilisha usajili wa dirisha dogo ndani ya muda uliopangwa.
Dirisha dogo la Usajili limefunguliwa leo Desemba 16 na litafungwa Janauri, 15, 2020 huku klabu zote zikipewa angalizo kukamilisha usajili kwa wakati kwa kuwa hakutakuwa na muda wa nyongeza.
Mbali na timu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara timu nyingine ni zile zinazoshiriki Ligi Daraja la Kwanza (FDL), LIgi Daraja la Pili (SDL) na Ligi ya Wanawake Tanzania (SWPL).

0 COMMENTS:
Post a Comment