Kaimu Mwenyekiti wa Simba, Mwina Kaduguda, amewatahadharisha wapinzani wao Yanga katika mchezo wao kama watakuja na maneno mengi basi ana uhakika watawafunga mabao matano.
Kaduguda ametoa kauli hiyo kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KMC, ikiwa zimebakia situ nne kabla ya Simba kucheza na Yanga Januari 4, Uwanja wa Taifa, Dar.
Simba itashuka kwenye mchezo huo ikiwa inaongoza ligi kwa pointi 31 baada ya kucheza mechi 12 wakati wapinzani wao Yanga wakiwa kwenye nafasi ya tatu na pointi 21 kufuatia kucheza mechi kumi kabla ya mchezo wa kesho Jumatatu dhidi ya Biashara United ya Mara.
Kaduguda alisema kuwa ubora wa timu yao umetokana na viongozi wa timu hiyo kutimiza wajibu wao huku akiwataka Yanga kuja kwa tahadhari kwenye mchezo huo kwa kuwa lazima wataibuka na ushindi.
“Timu inapata mafanikio kwa kuwa uongozi unafanya kazi kwa maelewano na kila mmoja amekuwa akitimiza majukumu yake maana ukiangalia tunahitaji kushinda kila mchezo ili tupate pointi tatu.
“Kiukweli watani wetu waje vizuri kwa sababu tunawaheshimu katika hali yoyote lakini lazima tuwafunge kwa kuwa tunaka ubingwa ili turudi kwenye michuano ya kimataifa lakini kama watakuja na mdomo, basi tutawafunga zile tano,” alisema Kaduguda.
0 COMMENTS:
Post a Comment