December 20, 2019


Kaimu mwenyekiti wa Simba, Mwina Kaduguda amesema kuwa ili kuhakikisha wanapata ushindi dhidi ya Yanga Januari 4, basi wachezaji wanatakiwa wasiidharau timu hiyo ambayo inatumia dirisha dogo kujipanga upya.

Simba na Yanga zinacheza kwa mara ya kwanza katika mzunguko wa kwanza wa ligi msimu huu, Januari 4, katika Uwanja wa Taifa jijini Dar.


Akizungumza na Spoti Xtra, Kaduguda alisema kuwa: “Wachezaji wanatakiwa waiheshimu Yanga pamoja na kuiona haipo sawa kwa sasa.

"Lakini watambue kuwa Yanga pindi inapocheza na Simba hubadilika kabisa wanakuwa timu nyingine na hawatacheza kama wanavyochezaga na Mtibwa au Mwadui, hivyo wanatakiwa waiheshimu Yanga.

"Lakini kubwa zaidi kwa upande wetu  kama Simba ni kuhakikisha tunapata ushindi dhidi yao."

4 COMMENTS:

  1. Simba wamebugi sana kumtimua ausems,huyo kocha mpya hajui lolote kuhusu timu maana yake hawezi kufanya usajili sahihi kulingana na mapungufu ya timu,ausems alipaswa aachwe afanye usajili dirisha dogo then ndio hayo maamuzi yakumtimua yangefuata,but all in all yanga na simba mnachemka sana kwenye masuala ya usajili.

    ReplyDelete
  2. Kajambe,kocha mpya Simba hata kazi hajaanza na wala bakuli fc msishughulike na kocha mpya wa Simba kiboko wa Yanga ni Matola subirini tano nyengine 5.

    ReplyDelete
  3. mi nadhani kama Simba SC kwa ukubwa wake ifike mahali tusiiwazie game moja na kuipa promo mingi tufanye hivyo hata kwa lipuli itakuwa na faida gani kumfunga yanga alafu tukapoteza kwa lipuli.....tuache uzamani.

    ReplyDelete
  4. Enter your comment...poit kubwa sana, yes siyo kuwazia yanga tu hata kama ni mechi ya watani but kuna mechi nyingine za kutiliwa mkazo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic