Baada ya watani zao wa jadi Yanga kuanza usajili kwa kasi, uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa Ofisa Habari wake, Haji Manara, umesema kamwe hautoweza kufanya usajili wa fasheni.
Manara ameeleza kuwa usajili ambao wanaufanya Yanga hauwezi kuwayumbisha nao wafanye usajili sababu ya mihemko ambayo haina maana.
Ameeleza kuwa Simba inasikiliza mapendekezo ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck na si kutazama kipi watani zao wa jadi wanafanya.
"Sisi hatuwezi kufanya usajili sababu ya wenzetu.
"Simba ni taasisi ambayo inafanya kazi kiueledi hivyo tunasubiri mapendekezo ya kocha wetu ndipo litafanyika hilo."
Kwa upande mwingine, Manara amesema wala hawatishwi na usajili ambao Yanga wanaufanya hivi sasa akiamini hauwezi kuwa na tishio kwao.
Kwani wabrazil ilikuwa chaguo LA kocha?
ReplyDeleteTimu haina washambuliaji. Tunaenda kupata aibu nyingine. Kocha mgeni atajuaje nafasi ya kuongeza dirisha dogo au apige ramli???
Tatizo la Haji ni usahaulifu na hili hapaswi kulaumiwa bali kuhurumiwa. Ni kweli simba inaelekea kuwa taasisi lakini tatizo la kuwa taasisi inayojielewa ni mifumo ambayo Yanga na Simba zimejiwekea na kuidumisha. Klabu hizi mbili zina siasa na tambo nyingi badala ya weledi kama anavyodai Haji Manara. Haji na kina Nugaz wanapaswa kujifunza toka kwa Senzo au hata kwa Zahera waachane na propaganda.
DeletePapara hazina baraka na mbio za sakafuni huishia ukingoni, walisema wa kale
ReplyDeleteUsajili wa Yanga ni magumashi matupu.
ReplyDeleteSimba wamebugi sana kumtimua ausems,huyo kocha mpya hajui lolote kuhusu timu maana yake hawezi kufanya usajili sahihi kulingana na mapungufu ya timu,ausems alipaswa aachwe afanye usajili dirisha dogo then ndio hayo maamuzi yakumtimua yangefuata,but all in all yanga na simba mnachemka sana kwenye masuala ya usajili.
ReplyDeleteHivi yanga inawasumbua nn jamani Mara usajali wamebugi Mara papara sawa fanyeni yenu mbona hamlali jamani kama wamebugi nyie hamjabugi shingilieni basi
ReplyDeleteSimba haina washambuliaji tangu aondoke okwi mambo yanaenda harijojo. Labda watu wamemsahau okwi.. yule ni mbishi..anarudi kukaba timu ikishambuliwa na timu ikipata mpira ni mwepesi na kasi mpaka wakati mwingine analazimisha mabeki wa timu pinzani kumfanyia rafu eneo la hatari. Kweli tutammiss sana.. sasa viongozi sijui hawajui hilo..naona wako kimya na timu imejaza viungo tuu..makocha ni wapya..waambiwe mapungufu mapema wayashughulikie..simba tunahitaji straika wa maana mmoja. Na kama tukiinasa ile nondo ya coast union itapendeza.. simba tuna beki mbrazili lakini kiukweli ukabaji wake sio mzuri..ni wa rafu mno..kimsingi unaweza kusema sio mkali kivile.
ReplyDeleteMashabiki wanashangaza.Timu haina washambuliaji!!Huku inaongoza kwa kufunga magoli mengi kuliko timu zote kwenye ligi!Mabeki wanadaiwa wabovu huku timu imefungwa magoli 3 mechi 10.Ikiwa ni rekodi. Watu wanalaumu bila ushahidi.Okwi ameondoka kwa kupenda mwenyewe wacheni kuendeleza ujinga wa kutegemea mchezaji mmoja.
ReplyDeleteSimba iliyofika robo final sio hii..sio ya kumuona kagere anastrugle peke yake mbele. Sasa sijui tunaenda mbele au nyuma.timu inashinda kwa shida..unasema inaongoza. Si ajabu hata kidogo kwa kutolewa hatua ya kwanza ligi ya mabingwa..mtu wa kazi pale mbele yuko mmoja tuu
ReplyDeleteNi kawaida mchezaji nambari 12 huwa anayo majibu yote likiwemo la mahala pa kumpeleka Moira ili kufunga goli nk tofauti na mchezaji Aliye uwanjani.
ReplyDeleteSisi mashabiki na wapenzi wa timu tuwe wenye Sunita kwa kuwaachia wataalamu nafasi ya kupanga Mambo kitaalam.