December 2, 2019

KIKOSI cha Yanga leo kina kazi nzito mbele ya KMC ambayo nayo inahaha kulipa kisasi cha kupoteza pointi sita zote msimu uliopita.

Yanga iliyo chini ya Boniface Mkwasa leo itashuka uwanja wa taifa kucheza na KMC ikiwa na kumbukumbu ya kushinda mechi zake zote mbili za msimu uliopita mbele ya KMC uwanja wa taifa.

Nahodha msaidizi wa Yanga, Juma Abdul amesema kuwa wachezaji wapo tayari kwa ajili ya kupambana wanawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi.

"Tunajua kwamba tuna kazi ngumu ya kufanya mbele ya mechi zetu ila kikubwa ambacho tunahitaji ni pointi tatu, mashabiki watupe sapoti," amesema.

Hasan Kabunda , nyota wa KMC amesema kuwa kila mechi kwao ni ngumu watapambana kupata matokeo bila hofu yoyote.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic