Mambo ni moto Simba, hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya uongozi wa Simba kutenga mamilioni ya usajili ambayo atakabidhiwa kocha mpya wa timu hiyo ambaye atatambulishwa keshokutwa Jumatano katika kipindi hiki cha dirisha dogo.
Uongozi huo chini ya mwekezaji, Mohammed Dewji ‘Mo’ umetenga Sh milioni 76 kwa ajili ya usajili ambazo itazitumia katika dirisha dogo litakalofunguliwa Desemba 16, mwaka huu.
Haya yamesemwa jana na uongozi wa timu hiyo katika mkutano mkuu wa wanachama wa klabu hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mhasibu wa Simba, Mathiew Asunga, akisoma mapato na matumizi ya klabu hiyo katika mkutano huo, alisema kuwa wametenga kiasi hicho cha Sh milioni 76 kwa ajili ya kukiimarisha kikosi cha timu hiyo katika kipindi hiki cha dirisha dogo.
“Bajeti ya msimu huu ni Sh bilioni 6.188 ambapo katika hiyo mapato ni bilioni 5.814 na matumizi ni bilioni 6.188 kukiwa na upungufu wa milioni 373.
“Hapo kuna mishahara ambapo ni bilioni 4.16 lakini kuna fedha za masoko milioni 52.4 na kuna maendeleo ya timu 241 na matumizi mbalimbali ni mil 123,” alisema Asunga.
Hadi sasa kocha anayepewa nafasi kubwa zaidi kuchukua mikoba hiyo ni Mzambia, Beston Chambeshi kama ambavyo Championi limekuwa likiripoti.








Huyu kocha hana CV ya kufundisha Simba.kumchukua huyu na kumuacha Aussem Ni sawa na kuruka mikojo na kukanyaga mavi...mwenye CV yake atuwekee hadharani maana hatutaki upigaji
ReplyDeleteHuyu kocha hana CV ya kufundisha Simba.kumchukua huyu na kumuacha Aussem Ni sawa na kuruka mikojo na kukanyaga mavi...mwenye CV yake atuwekee hadharani maana hatutaki upigaji
ReplyDeletehaya sasa maigizo yan kocho was Nkana tulioipiga tukiwa na uchebe Leo aje simba haiwezekani jaman tuangalie kocha atakae isaidia simba kufika pale tulipo ishia mwaka Jana naikiwezeka tuvuke hapo
ReplyDeleteMbona huyo akiwa Nkana aliipiga Ud songo nje ndani...hao Ud songo ambai walitupiga sisi.Kocha hapimwi hivyo
DeleteUzushi tu huo. Huyo hayupo katika orodha ya makocha wanaotakiwa na Simba.
ReplyDeleteSio kocha mbaya. Wacheni kukariri. Alifundisha Chipolopolo.Timu ya Taifa ya Zambia .
ReplyDeleteaje tu,tatizo sio kocha ni wachezaji wenyewe na starehe zao.
ReplyDeleteaje tu,tatizo sio kocha ni wachezaji wenyewe na starehe zao.
ReplyDeleteNi Kocha mzuri sana tu. Kikosi cha Uchebe cha Simba kichoifunga Nkana akama kingekuwa chini ya mzambia huyu kingefika fainali na wala Simba isingepigwa hamsa hamsa.
ReplyDelete