KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck leo yupo benchi kwa mara ya kwanza akiongoza kikosi chake kinachomenyana na Arusha FC mchezo wa Kombe la Shirikisho Uwanja wa Uhuru.
Mpira umemalizika uwanja wa Uhuru kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Arusha United
Dakika ya 18 Clatous Chama anafunga bao la kuongoza baada ya mlinda mlango wa AFC kutema shuti lililopigwa na Meddie Kagere.
Dakika ya 24 kiungo wa Simba, Gerson Fraga anafunga bao la pili kwa Simba akiwa nje ya 18 akimalizia pasi ya Ibrahim Ajibu.
Dakika ya 27 Deo Kanda anapachika bao la tatu akiwa ndani ya 18 akimalizia asisiti ya Ibrahim Ajibu.
Dakika ya 33 Ibrahim Ajibu anafunga bao la nne akimalizia pasi ya Chama akiwa ndani ya 18.
Kagere anapachika bao la tano dakika ya 57 akiwa ndani ya 18 baada ya mlinda mlango kutema shuti lililopigwa na Kahata.
Wilker da Silver anaingia dakika ya 57 akichukua nafasi ya Kagere
Chama anatoka dakika ya 58 anaingia Shiboub
Keneddy Juma anaingia pia kuchukua nafasi ya Shomari Kapombe.
Dakika ya 66 Kahata anafunga bao la sita akimalizia asisti ya Deo Kanda
duh manara alisema kweli hii mechi ngumu kweli kweli,naona hapa simba wanaomba mpira uishe haraka,duh !!!!!!!
ReplyDeletePiga nane hao 8
ReplyDeleteHata 10 watapigwa 2
ReplyDeleteHawa mwaka jana walitupa taabu sana mwaka huu watajuta sana mpaka sasa goli 4
ReplyDeleteBado 2 hapo
ReplyDeleteUjumbe kwa vyura huo
ReplyDeleteKwanza hongera kwa ushindi,ila tunapaswa kujua timu tuliyocheza nayo sio level yetu tusije kujisahau nakujiona tuko vizuri,myself ningeshauri mwalimu aendelee kukisoma kikosi kwa mapana zaidi bado kuna mapungufu mengi sana difense haijakaa sawa,ila ninachoamin within 4 matches mambo yatakaa sawa,mungu ibariki simba na mungu libariki benchi la ufundi la simba.
ReplyDeletemawazo yenu mazur ila tambuen kuna wachezaji kadhaa wa kikosi cha kwanza hawapo so timu haiwez kuwa na rithim mliyoizoea na ujio wa kocha mpya pia timu inaitaj mechi 3 au 4 kuwa sawa ila niwaondoe wasiwasi tarehe 4 timu itakuwa sawa na mtafurahii sna
ReplyDelete