December 28, 2019


UONGOZI wa Simba umesema kuwa mlinda mlango wa KMC, Jonathan Nahimana leo alikuwa kikwazo kikubwa kwao kwa kuzuia idadi ya mabao ambayo yalikuwa yanalilenga lango mwanzo mwisho licha ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

KMC leo iliwakaribisha Simba kwenye mchezo wa ligi uliochezwa uwanja wa Uhuru imekubali kichapo cha mabao 2-0 na yote yalifungwa kipindi cha pili.

Ofisa wa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa walikuwa na nafasi ya kufunga mabao mengi ila uimara wa mlinda mlango wa KMC umezuia idadi ya mabao ambayo wameyazoea kwa Simba.

"Tulikuwa na nafasi ya kufunga mabao mengi ila uimara wa mlinda mlango wa KMC umefanya mashambulizi mengi kutozaa matunda, yote kwa yote muhimu kwetu pointi tatu," amesema.

Mabao ya Simba yalifungwa na Deo Kanda dakika ya 46 akimalizia pasi Hassan Dilunga  la pili lilifungwa na Gerson Fraga aliyefunga bao hilo akiwa nje ya 18 dakika ya 90+3 kwa pasi ya Francis Kahata.

Ushindi huo unaifanya Simba kujikita kileleni baada ya kucheza mechi 12 ikiwa na pointi 31  na KMC kusalia nafasi ya 17 ikiwa na pointi tisa kibindoni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic