December 29, 2019


Homa inapanda aisee! Kuelekea kwenye mchezo wa Kariakoo Derby ambao utapigwa Jumamosi ijayo, Simba mapema tu wameshaweka mkatakati wao kuhakikisha wanawalaza mapema tu watani zao, Yanga. 

Simba inayoongoza ligi kwa pointi 28, inatarajia kucheza na Yanga inayokamata nafasi ya tisa ikiwa na pointi 18, Januari 4, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar. Yanga jana ilitarajiwa kucheza na Prisons katika mchezo wa ligi.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa, alisema ameamua kuwahi kurejea nchini akitokea Afrika Kusini ambako ni nyumbani kwake kutokana na ugumu wa mchezo dhidi ya Yanga, hivyo sasa wapo kwenye mkakati mzito wa kuhakikisha wanapata ushindi.

“Najua mechi ya Yanga siyo kama mechi nyingine licha ya zote kuwa na pointi tatu kwa sababu hii ni mechi inayokutanisha watani wa jadi na kinachoangaliwa ni matokeo ya ushindi ndiyo jambo kubwa na ndiyo maana nimewahi kurejea kutoka Afrika Kusini kwa ajili ya kuweka mambo sawa.

“Mikakati na mipango imeshakuwa tayari kuelekea mchezo huo lakini hatuwezi kuweka wazi kwa sasa kutokana na kuhofia kuwavuruga wachezaji wetu ikizingatiwa tuna mechi moja kesho (leo) dhidi ya KMC lakini baada ya mchezo huo kila kitu kitakuwa wazi kwa kuwa tunakata ushindi,” alisema Mazingisa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic