December 28, 2019


MCHEZO wa Ligi Kuu Bara kati ya KMC na Simba uwanja wa Uhuru umekamilika.

Simba imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kusepa jumla na pointi tatu.

Deo Kanda dakika ya 46 anafunga bao la kuongoza kwa Simba kwa guu la kulia akimalizia asisiti ya Hassan Dilunga, kipindi cha pili Fraga anafunga bao la pili dakika ya 90+3 akimalizia pasi ya Kahata.

Mashabiki wamejitokeza kiasi chake kuutazama mchezo wa leo.

Deo Kanda anaonyeshwa kadi ya njano dakika ya 15 na mwamuzi.

Boniface Maganga wa KMC anaonyeshwa kadi ya njano dakika ya 50.

Serge anaingia dakika ya 60 kwa KMC akichukua nafasi ya Maganga ambaye ameumia.

Dakika ya 63 Clatous Chama anaingia anachukua nafasi ya Ibrahim Ajibu.

Hassan Dilunga anaoka nje dakika ya 68 anaingia Francis Kahata.

Mzamiru Yassin anaonyeshwa kadi ya njano dakika ya 79 kwa kumchezea rafu Kabunda.

Kanda anakosa nafasi ya wazi dakika ya 87 akiwa ndani ya 18 kwa kupaisha mpira juu.

3 COMMENTS:

  1. Uwe unaweka na vikosi vya timu nyingine Kama leo KMC haujaweka kikosi Chao.Mara nyingi unaweka vikosi vya Simba na yanga tu hizo timu zingine ukiweka vikosi vyao unapungukiwa nin?

    ReplyDelete
  2. kweli huyu jamaa anaboa kweli yani anatoa kikosi kimojatu sijui kwaninitu

    ReplyDelete
  3. Bora muongelee ushidi wa Mnyama

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic