LIVERPOOL
wamekutana na kichapo cha mwaka baada ya kuchapwa mabao 5-0 na Aston Villa
katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Carabao uliochezwa jana Jumanne.
Liverpool
walichezesha wachezaji wengi ambao umri wao ni chini ya miaka 19 kwenye mchezo
huo kutokana na timu ya wakubwa kwenda kwenye mchezo wa Klabu Bingwa Dunia
nchini Qatar.
Kocha wa
Liverpool, Juggen Klopp aliomba mchezo huo usogezwe mbele lakini FA wakagoma na
akaamua kupeleka vijana ambao wamekutana na kichapo hicho.
Villa ambao
walikuwa wanatumia zaidi uzoefu kwenye mchezo huo walipata mabao yao kupitia
kwa Conor Hourihane dakika ya 14, Morgan Boyes (alijifunga dakika ya 17), Jonathan
Kodjia (37 na 45) na Wesley Moraes (90).
Kocha wa
Liverpool chini ya miaka 23 ambaye alikuwa anaisimamia timu hiyo, Neil
Critchley, amesema kuwa anakubaliana na kichapo hicho, lakini anaamini kuwa
wachezaji wake wamejifunza kitu kwenye mchezo huo uliopigwa kwenye Dimba la Villa
Park.
“Tumekutana
na timu kubwa England, wachezaji wangu wengi hawakuwa na uzoefu na hilo ndiyo
limetusumbua, naamini kuwa watakuwa wamejifunza kitu kipya,” alisema kocha
huyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment