UONGOZI wa Yanga umefikia makubaliano ya pamoja
kumtoa kwa mkopo beki wake wa pembeni Muharami Issa ‘Marcelo’ kwenye usajili wa
dirisha dogo lililofunguliwa Desemba 16.
Marcelo alijiunga na Yanga kwenye msimu huu wa Ligi
Kuu Bara akitokea Singida United baada ya aliyekuwa beki wa timu hiyo Gadiel
Michael kuachana na timu hiyo msimu uliopita.
Habari zinaeleza kuwa
beki huyo amefikia makubaliano ya kutolewa kwa mkopo kwenda Singida
United alipochukuliwa na Yanga kutokana na kukosa namba ndani ya kikosi cha kwanza.Ofisa Habari wa Singida United, Cales Catemana amesema kuwa mpango mkubwa uliopo ndani ya kikosi hicho ni kukirejesha kwenye ukali wake wa zamani.
Safari njema
ReplyDelete