December 19, 2019


Rasmi uongozi wa Yanga umethibitisha kuwa unakamilisha usajili wa kiungo mchezeshaji fundi wa AS Kigali ya Rwanda, Haruna Niyonzima ambaye siku yoyote kuanzia leo Jumatano atatua nchini kufanikisha usajili wake.

Niyonzima aliwahi kuichezea Yanga kwa mafanikio makubwa akichukua mataji matatu mfululizo ya Ligi Kuu Bara huku akibeba Kombe la Kagame na Kombe la FA.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatano, uongozi wa Yanga umeshafikia makubaliano mazuri ambayo yana asilimia 100 na kiungo huyo.

Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla akizungumza na viongozi wa Baraza la Wazee la timu hiyo juzi alisema kuwa wapo kwenye mchakato wa mwisho kabisa wa kumchukua kiungo huyo mahiri.


Mtoa taarifa aliliambia Championi kuwa wazee walishangilia sana baada ya kuelezwa kuwa Niyonzima anarejea tena Jangwani hali ambayo inaonyesha kuwa ni kipenzi chao.

“Katika kikao tulichofanya kati yetu sisi Wazee wa Yanga na viongozi, mengi yamejadiliwa na kati ya hayo ni hili zoezi la usajili linaloendelea ni baada ya viongozi kututhibitishia mengi mazuri lakini kati ya hayo ni hili la kumrejesha Niyonzima.

“Kiukweli sisi Wazee wa Yanga tulifurahi sana, ipo wazi Niyonzima ni kati ya viungo bora Afrika Mashariki na Kati, hatukuwa na kiungo mchezeshaji mwenye uwezo mkubwa wa kumiliki mpira na kupiga pasi za mabao.

“Hivyo kurejea kwake kumetufanya sisi wazee kupata morali ya kwenda uwanjani kuiangalia timu yetu itakapokuwa ikicheza mechi zake za ligi ikiwemo ile na watani wetu wa jadi, Simba,” alisema mtoa taarifa huyo.

Msolla hivi karibuni alithibitisha kufanya mazungumzo na Niyonzima huku akisema kuwa: “Niyonzima ni kati ya wachezaji waliopo kwenye mipango yetu na kama mipango ikikaa sawa, basi atajiunga na Yanga katika dirisha dogo.”

Imeelezwa kuwa timu hiyo imemwandalia Niyonzima mkataba wa miaka miwili, wakiamini kuwa atakuwa msaada mkubwa kwao kwenye mechi dhidi ya Simba, Januari 4.

Pia kiungo huyo karibuni alikiri kufanya mazungumzo na Yanga na kuwa anatamani kurejea klabuni hapo.

5 COMMENTS:

  1. Mazungumzo yanaendelea vizuri na niyonzima ametoa sharti ambalo viongozi wa yanga hawajui watalitekeleza vipi , yeye amesema yuko tayari kusaini yanga bure lakini apewe ile jezi ya jina lake waliyoichoma moto ikiwa katika uhalisia wake

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni jezi ya Niyonzima au ya shabiki alieamua kuandika jina la Niyonzima🤔

      Delete
  2. Imetufurahisha Sana na tumshukuru Mungu kuwa anajiunga Bila ya malipo kutokana na mapenzi yake na Yanga am ambalo ni faraja isiyo na mfano na sisi tunahitaji wa hezaji wenye moyo kama huyu kijana.

    ReplyDelete
  3. Ni vyema niyonzima kurudi. Viongozi wafuatilie na uwezo wa kamsoko kama unafaa wampe mkataba wa msimu mmoja. Chilwa naye anakwenda kubakiza miezi 6 waanze mazungumzo naye.

    ReplyDelete
  4. wanakumbuka majkombo duuu kufulia kubaya

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic