December 19, 2019


TIMU ya Polisi Tanzania imefunguka kuwa inahitaji kuongeza wachezaji wanne katika usajili wa dirisha dogo lilofunguliwa Desemba 16 ili kuongeza nguvu katika kikosi hicho.
Polisi ambayo awali ilikuwa inafundishwa na Seleman Matola aliyetimkia Simba, inahitaji kuongeza nafasi ya kiungo na ushambuliaji ambayo ndiyo ilionekana kuwa na mapungufu.

Ofisa Habari wa Polisi, Frank Lukwaro amesema kuwa, baada ya kumalizana na aliyekuwa mchezaji wa Yanga Pius Buswita aliyesaini mkataba wa miezi sita, bado wanahitaji kuongeza nguvu kwa kusajili majembe wengine watatu ambao wapo katika mazungumzo nao.
“Tunahitaji kusajili wachezaji wanne katika nafasi za kiungo na mshambuliaji , tumelenga zaidi wachezaji ambao hawana mikataba," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic