SVEN Vanderbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa mashabiki wasiwe na haraka ya kupata matokeo makubwa kwani kazi ndo kwanza inaanza.
Kocha huyo aliyepokea mikoba kutoka kwa Patrick Aussems ameiongoza Simba kwenye mechi tatu na kukusanya jumla ya mabao 12 ambapo alianza kwa ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Arusha FC kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho na alishinda mabao 4-0 dhidi ya Lipuli na mbele ya KMC aliibuka na ushindi wa mabao 2-0 ilikuwa ni mechi za ligi zote zilichezwa uwanja wa Uhuru.
"Bado kikosi kinaimarika taratibu na wakati ukifika kila mmoja atapenda kuona namna timu inavyopambana na kufikia mafanikio ambayo tunayahitaji," amesema.
Simba ni kinara ndani ya ligi akiwa na pointi 31 na amecheza jumla ya mechi 12, kesho atapambana na Ndanda FC mchezo utakaochezwa uwanja wa Uhuru.
0 COMMENTS:
Post a Comment