Pombe imemponza askari wa polisi na kusababisha kukatishwa uhai wake kutokana na ugomvi ulioibuka baina yake na wahudumu wa baa ambao walimpiga kichwani na fimbo maalumu ya kuchezea ‘pool table’.
Tukio hilo ambalo lilitokea katika baa mojawapo iliyopo maeneo ya Kibera katika makazi duni jijini Nairobi, imeelezwa kuwa lilisababishwa na ugomvi wa kuwania bia kati yao.
Taarifa ya Jeshi la Polisi nchini humo, imeeleza kuwa mwili wa ofi sa huyo wa polisi ulipatikana katika gari lake ambapo alikuwa ametembea kwenda kupanda baada kupigana na wahudumu hao.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, tayari polisi wanawashikilia watuhumiwa wawili kuhusiana na mauaji hayo.
Inadaiwa ofi sa huyo aligongwa kichwani na mhudumu wa baa hiyo na kumsababishia majeraha ambapo damu ilivilia ndani ya ubongo, hali iliyosababisha kukumbwa na umauti alipoingia ndani ya gari yake.
“Alitembea kuelekea kwenye gari baada ya kujeruhiwa. Alitokwa na damu na kufariki ndani ya gari,” alisema shuhuda mmoja ambaye alisaidia kuondoa mwili huo kwenye gari.
Polisi walitembelea baa hiyo na kupata fi mbo hiyo ya kuchezea pool table ambayo inasadikika kutumika kumpiga nayo kichwani wiki iliyopita.
Mashuhuda walilieleza jeshi la polisi kuwa wawili hao walikuwa wametofautiana katika baa juu ya chupa ya bia. Washtakiwa hao wawili walipandishwa kizimbani Ijumaa iliyopita na polisi waliruhusiwa kuwaweka kizuizini kwa wiki nzima hadi uchunguzi utakapokamilika.
0 COMMENTS:
Post a Comment