December 26, 2019


RASMI mchezo kati ya Tanzania Prisons na Yanga uliotakiwa kuchezwa kesho uwanja wa Sokoine, Mbeya utahamia uwanja wa Samora uliopo Iringa.

Uwanja wa Sokoine umezuiwa na Bodi ya Ligi ya Tanzania kutumika kwa sasa kutokana na kutokuwa katika hali nzuri baada ya usiku wa leo kufanyika tamasha la muziki ambalo limesababisha uharibifu mkubwa wa sehemu ya kuchezea.

Tanzania Prisons watakuwa wenyeji kwenye mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani kutokana na kila mmoja kupania kupata pointi tatu.

Tanzania Prisons ina pointi 20 mpaka sasa haijapoteza mechi hata mja ndani ya ligi kati ya mechi 12 ilizocheza ikiwa imeshind nne na kutoa sare nane huku Yanga ikiwa imepoteza mechi moja na imeshinda tano na ina sare nne ikiwa na pointi 18

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic