Kaimu mwenyekiti wa Simba,Mwina Kaduguda amewataka wanachama wa Simba kuhakikisha wanazitumia vyema kadi za kisasa ili kuongeza kipato cha klabu hiyo.
Amesema Simba ina kiu ya kuchukua mataji ya ubingwa wa Ligi Kuu bara na hata ubingwa wa Afrika, hivyo zinahitajika pesa za kutosha kuendesha klabu hiyo.
"Tunahitaji kuiangusha TP Mazembe na hatuwezi kufanikiwa kwa maneno maneno, vinatakiwa vitendo ndio maana tumebuni kadi za kisasa ambazo zitakuwa zinatuingizia pesa.Lazima tubadilike kuhakikisha tunafanya mambo kisasa ili tufanye makubwa Afrika.
"Tukawe mabalozi kwa wengine ambao hawajafika hapa maana pamoja na klabu kunufaika pia mnaweza kukopeshwa bodaboda na bajaji," amesema Kaduguda.
Idadi ya wanachama waliojitokeza katika uzinduzi huo ilikuwa ndogo huku sababu ikitajwa kwamba hawakutangazwa ipasavyo kwa kuhofia vurugu.
Kumbe mnauziwa bodaboda kijanja? lkn Kaduguda umetumwa uzungumze mbona ujasema malipo ya kazi tunalipia akaunti gani tujue,akaunti yake Simba au ya Mo Dewj?
ReplyDeleteYa Mo Dewji, kwan shida yako nn? as account yeyotee tunalipaa..mpaka utapike nyongo
ReplyDeleteBiashara ni matangazo
ReplyDeleteElimu inahitajika zaidi kwa wapenzi na wanachama wa simba sc kujua faida zitokanazo na card hii pia naamini wengi watachukua kikubwa ni kuwa na subra tu kwani siku zote mwanzo ni mgumu ila naamini kadri siku zitakavyokua zikisonga na idadi ya watakaochukua itaongezea.....simba sc nguvu moja
ReplyDeletesimkatembeze bakuli tu; hizi kadi za kisasa na bakuli vinatofauti gani?
ReplyDelete